Picha askari wa kutuliza ghasia akiwa tayari kwa mapambano n awananchi wa zanzibar ambao inasemekana walivamia kituo cha polisi wakiwa na silaha za jadi kama vile rungu na mapanga |
Wananchi wa Zanzibar wakiwa kwenye maandamano wakati wakielekea kituo cha polisi na kabla machozi ya mabomu hayajaanza kulipuliwa na askari.Picha Zote na Abdulaziz El Shuwehdy |
JANA JIONI KUNDI KUBWA LA WATU WANAOLIUNGANISHA KUNDI LIFAHAMIKALO KWA JINA LA UAMSHO,AMBALO LIMEKUWA LIKIUPIGA VITA MUUNGANO WA TANZANIA NA ZANZIBAR,LILIVAMIA KITUO KIKUU CHA POLISI CHA MADEMA KISIWANI HUMO JIONI YA JANA NA KUSABABISHA VURUGU KUBWA,WAKITAKA KUACHILIWA KWA KIONGOZI WAO ALIEKAMATWA JIONI YA JANA KWA KUONGOZA MHADHARA BILA YA KUWA NA KIBALI CHA SERIKALI.
HALI HIYO IMESABABISHA VURUGU KUBWA KITUONI HAPO HUKU ASKARI POLISI WA KITUO HICHO WAKILAZIMIKA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI ILI KUWATAWANYA WATU HAO AMBAO WENGI WAO WAKO NA SILAHA ZA JADI AMBAZO NI MARUNGU,MAPANGA NA MAWE ILI KUPAMBANA NA ASKARI POLISI KITUONI HAPO VURUGU HIZO ZIMEENDELEA TENA ASUBUHI YA LEO.
No comments:
Post a Comment