Wednesday, May 23, 2012

SHAMRA SHAMRA ZA USHINDI WA ZITTO KATKA UCHAGUZI DARUSO-MUCE

Wadau wakijipongeza baada ya ushindi wa MTAMA(ZITTO) katika uchaguzi wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam kitivo cha uwalimu MUCE- IRINGA siku ya Jumatatu
Baada ya kampeni zilizo dumu kwa wiki moja, wanafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam kitivo cha uwalimu Iringa (MUCE) walifanya uchaguzi siku ya Jumatatu tarehe 21may 2012, Kwa hali ya amani na utulivu wa hali ya juu na hatimaye kuwapata viongozi wa serikali yao, Uchaguzi huo uliokuwa unawagombea zaidi ya watano katika kila nafasi ulilazimu kuwachukuwa siku nzima kufanyika na hatimaye Bw. Mtama J aka ZITTO aliibuka mshindi katika nafasi ya urais, Aidha reporter wetu ana habari zaidi,,,!!
Wana MUCE walipokuwa wamejipanga kunda kufanya uchaguzi siku ya jumatatu wiki hii
Harakati za uchaguzi zikiendelea chuoni hapo
Baada ya uchaguzi wanafunzi wa MUCE wakisubiri matokeo kwa hamu kubwa
Wadau wakisubiri matokeo baada yakutoka kuchagua kiongozi wa mtakae
Wanadada nao hawa kuwa nyuma katika uchaguzi huu
Wanafunzi wa MUCE wakifuatilia kwamakini matokeo ya uchaguzi yalipokuwa yanatangazwa na mwenyekiti mratibu wa uchaguzi DARUSO MUCE-IRINGA
Shamra shamra za ushindi wa Mtama mara tu baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa urais DARUSO-MUCE
Wadau walipo mbeba juu juu Mtama J. aka ZITTO mara baada ya kutangazwa mshindi wa urais MUCE
Mtama na Makamu wake wa urais mara baada ya kutangazwa kuwa washindi wa uchaguzi uliofanyika jumatatu chuo kikuu MUCE-IRINGA
Picha ya juu na chini ni sherehe za kuwapongeza wa shindi wa uchaguzi na viongozi wapya wa DARUSO-MUCE-IRINGA

No comments:

Post a Comment