Tuesday, May 29, 2012

WAZAZI NA WALIMU WAKEMEA VIKALI VURUGU ZILIZOTOKEA SHULENI IKUNGI, SINGIDA.


Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi jimbo la Singida mashariki,Olvary Kamilly,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) juu ya baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo,kuaguka na kuzirai wakiwa shuleni.Picha na Nathaniel Limu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi,mwalimu Kamilly,alisema vurugu zilizokuwa zinasababishwa na baadhi ya watu ambao wengi wao wakiwa hawana wanafunzi shuleni hapo,sasa hazipo tena.
“Nikuambie tu kwamba kwa sasa hali ni shwari,amani na utulivu sasa vimerejea.Mahudhurio ya wanafunzi hapa shuleni,yamerejea kama kawaida yake ya asilimia kati ya 97 na 99″,alisema mwalimu Kamilly.
Baada ya kufanyika kwa mkutano mkuu maalum wa wazazi hivi karibuni, pamoja na kujadili kwa kina tatizo la baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo kuanguka na kuzirai,mkutano huo ulikemea vikali vurugu zilizokuwa zikifanywa na kikundi cha watu dhidi ya uongozi wa shule hiyo.
Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka idara ya elimu wilaya akiwemo afisa elimu wilaya,Patrick Mwaluli, uliagiza pia mtu/watu watakaowazuia tena wanafunzi kuhudhuria shule, pamoja na wale watakaobainika kuleta fujo shuleni,wachukuliwe hatua za kisheria.

No comments:

Post a Comment