WAZAZI WA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI IKUNGI MKOANI SINGIDA WAFANYA MKUTANO MAALUM KUJADILI TATIZO LA WANAFUNZI KUZIRAI.
Mkuu
wa shule ya msingi ya Ikungi jimbo la Singida Mashariki akitoa taarifa
yake ya kuanguka na kuzirai kwa baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo mbele
ya mkutano mkuu maalum wa wazazi/walezi.
Kada
wa CHADEMA Hussein Mwangia akizungumza kwenye mkutano mkuu maalum wa
wazazi/walezi ulioitishwa kwa ajili ya kujadili tatizo la kuanguka na
kuzirai kwa wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi jimbo la Singida
Mashariki.
Mwenyekiti
Mstaafu wa CCM mkoa wa Singida Sumbu Galawa akitoa nasaha zake kwenye
mkutano mkuu maalum wa wazazi/walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi
Ikungi kuhusu tatizo la kuanguka na kuzira kwa wanafunzi.
Baadhi
ya wazazi/walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi waliohudhuria mkutano
mkuu maalum kujadili tatizo la kuanguka na kuzirai kwa wanafunzi. (Picha
zote na Nathaniel Limu).
Na.Nathaniel Limu.
Busara
za Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Singida Mzee Sumbu Galawa
zimenusuru kuvunjika kwa mkutano maalum wa wazazi wa wanafunzi wa shule
ya msingi Ikungi jimbo la Singida Mashariki.
Mkutano
huo uliitishwa na uongozi wa shule hiyo na kamati yake, kwa ajili ya
kujadili na kulitafutia ufumbuzi tatizo la baadhi ya wanafunzi kuanguka
na kuzirai.
Dalili
zilianza kujionyesha mapema kwamba mkutano huo usingemalizika salama,
kutokana na kuwepo kwa kikundi ambacho kilidhamiria mwalimu mkuu wa
shule hiyo Olvary Kamilly, anaondolewa katika shule hiyo.
Kiongozi
wa Kikundi hicho kinachodaiwa ni cha wanachama wa CHADEMA Husseini
Mwangia, kabla hata mwenyekiti wa kamati ya shule Naftali Gukwi
hajafungua mkutano, alikuwa akilazimisha apewe nafasi ya kuzungumza.
Baada
ya mwenyekiti Gukwi kufungua mkutano huo, alimruhusu Hussein Mwangia
ambaye ilidaiwa kuwa hana mtoto anayesoma katika shule hiyo, kuzungumza.
Mwangia
baada ya kuruhusiwa, huku akionyesha wazi kujawa na jaziba nyingi,
alianza kutoa tuhuma mbali mbali kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na
mwenyekiti wa kamati.
Mwangia
ambaye alichukua muda wa dakika 52 kuporomosha tuhuma hizo badala ya
kuzungumzia mada pekee ya mkutano huo, alimtuhumu mwalimu mkuu kuwa
hana ushirikiano na wazazi.
Aidha,
alidai kuwa mwalimu huyo aliwahi kusema kuwa shule hiyo sio mali ya
wazazi bali ni mali ya halmashauri ya wilaya ya Singida.
Baada
ya mkutano huuo kuonyesha dalili za wazi kuwa amani na utulivu haipo
tena wakati Mwangia akizungumza, mzee Galawa alipewa nafasi kutoa nasaha
zake.
Mzee
Galawa alisema kuwa jazba ikitawala mahalai po pote, huwa haijengi wala
haitatui tatizo, bali hubomoa, kuongeza makali ya tatizo husika na
mbaya zaidi, huchonganisha watu.
Kwa
upande wake Jumanne Ngaa, yeye alipigilia msumari wa mwisho baada ya
kusema kuwa wengi wa watu wanaoshinikiza mwalimu mkuu aondoloewe, hawana
wanafunzi katika shule hiyo na kuwa lengo lao ni kutafuta umaarufu kwa
siasa.
Baada
ya maneno hayo, Mwangia alibaini kuwa upepo haupo tena upande wao,na
hivyo aliwaamuru wanakikundi wenzake kususia mkutano huo na kuondoka
mahali hapo.
Kabla
ya kufungwa kwa mkutano huo, viongozi wa madhehebu ya dini za Kiislamu
na Kikristo, walifanya sala ya kumwomba Mwenyezi Mungu, asaidie
kuliondoa tatizo la kuanguka kwa wanafunzi.
Hello to every , because I am truly keen of reading this website's post to
ReplyDeletebe updated regularly. It consists of nice stuff.
Take a look at my web-site; emergency wind damage repair Services north carolinas