Wednesday, May 9, 2012

SIMBA YAONDOKA KWENDA SUDAN LEO

Makamu mwenyekiti wa timu ya Simba Bw. Godifrey Nyange ''Kaburu''akionyesha ishara ya vidole vitano na mchezaji nyota wa timu hiyo Emmanueli Okwi, kwa kuonyesha  alama hii huenda walikuwa wakimaanisha ushindi wa magoli 5 walioupata baada ya kuwafunga  watani wao timu ya Yanga .hii ilikuwa katika uwanja wa ndege wa mwalimu juliasi Nyerere jijini Dar es salaam wakati timu hiyo ikijianda kuondoka kwenda Sudani kwenye mchezo wao wa marudio na Al Hilal Shandy jumapili ijayo.


Kapteni wa timu ya Simba Juma Kaseja akihojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya timu hiyo.Makamu mwenyekiti wa timu ya simba Bw;Godifrey Nyange ''Kaburu akiteta jambo na wachezaji wa timu ya Simba.


Wachezaji wa timu ya Simba wakiingia kwenye chumba maalumu tayari kwa kuondoka.

No comments:

Post a Comment