Thursday, May 31, 2012

MAZISHI YA MWANAFUNZI WA ARDHI UNV. AGUSTINO MBIKILWA AKA TINO TINOLA

Mwili wa The Late Agustino Mbikilwa ( TINO TINOLA) ukitoka katika viwanja vya chuo kikuu cha Ardhi ambapo uliletwa kwaajiliya kuagwa rasim na wanafunzi na walimu wachuoni hapo siku ya Jumaanne tarehe 29 May 2012 na baadaye kurejeshwa nyumbani kwao Tegeta tayari kwa mazishi yaliofanyika siku ya Jumatano, 30 may 2012,
REST IN PEACE TINO TINOLA
Maisha ni safari na safari hufika siku ikafika kikomo na hapo ndipo tunapo rejea kwa Muumba, Yaani kule tuliko toka,,,,!! Katika hali ya huzuni na majonzi makubwa wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo Ifm, Udsm, Cbe, Ardhi na vingine vingi walishiriki katika mazishi ya kumwaaga mwanafunzi wenzao aliyefariki dunia kwa ajali ya gari usiku wakuamkia Jumamosi May 26  AGUSTINO MBIKILWA alimaarufu TINO TINOLA,,
Mimi Binasfi nilimjua Tino sio tuu kama rafiki lakini ni kama ndugu,, Kwa mara ya kwanza nakutana na Tino ilikuwa ni shule ya msingi na urafiki wetu ulidumu kutoka utoto paka hii leo,,, Na kwa mara ya mwisho naongea na Tino ilikuwa ni siku moja kabla sijaja masomoni alipo kuja nyumbani kunitembelea.
Tino alikuwa ni mcheshi, mwenye busara na mkarimu, Alipenda sana kucheza mpira wa miguu na hiyo ndio iliokuwa ikimpa jina kubwa na umaarufu kila shule aliyo soma na popote alipo ishi,
Watatu kutoka kushoto  Tino na timu ya Chuo kikuu Ardhi
Tino alijulikana kama mfungaji bora katika kikosi cha soka cha Mbezi Beach Sec (2007-09) alipokuwa amemalizia kidato cha sita, Aidha umahiri wa Tino ulionekana hata kwenye jamii inayo mzunguka, Tino alikuwa mchezaji bora wa timu ya vijana kitaani ( Mkanada Youth Football Star),
Tino ambaye alimaliza kidato cha sita 2009 na kujiunga na chuo kikuu cha Ardhi kwa shahada ya kwanza aliendelea kuwa mfano wakuigwa kwa wanafunzi wa chuoni hapo kwa kudumisha urafiki kwa njia mbali mbali hasa katika michezo na darasani,,,!!
Tino enzi za uhai wake
TINO alikuwa mchango mkubwa sana kwangu ijapokuwa hatukuwa na muda mwingi wakukaa na kuzungumza kutokana na ratiba za majukumu ya maisha ila Katika marafiki nilio wahi kusoma nao TINO NI RAFIKI YANGU WA KWELI,,
 REST IN PEACE TINO TINOLA








Katika safari ya kumsindikiza Ndugu yetu, rafiki na mwanafunzi mwenzetu AGUSTINO MBIKILWA aka (TINO TINOLA) katika nyumba yake ya milele hali.
WANAFUNZI WA VYUO MBALIMBALI JIJINI DAR ES SALAAM PAMOJA NA WANAJAMII WAKARIBU WAKITOA SALA YA KUMWAAGA RAFIKI NA KIPENZI CHETU AGUSTINO MBIKILWA KATIKA KANSA LA KATOLIKI WAZO HILL TEGETA JANA JUMATANO
Baadhi ya wanafunzi mbalimbali wachuo kikuu cha Ardhi na Classmate wa marehemu Tino katika mazishi ya Tino Tinola yalio fanyika jana katika makaburi ya Wazo Hill Tegeta Da es salaam
Baadhi ya wanafunzi waliomaliza na Tino shule ya msing 2001, wakijadiliana jinsi ya kuunda chama cha Kunduchi Alumin kitakacho wakutanisha na kusaidiana katika shida na raha. Wanajadili hayo yalipokutana nyumbani kwa kina marehemu Agustino mbikilwa siku ya jumatatu, Hili pia lilikuwa ni wazo za Tino kabla ajakutwa na mauti.
Wanafunzi wa kibeba jeneza la kipenzi chao na rafiki wakaribu  Marehemu Agustino Mbikilwa walipo kuwa wanaelekea makaburini,
Hiyo ndo nyumba ya milemile ya marehemu Agustino Mungu aiweke roho yake mahal pema pepon Eiiiiimen

No comments:

Post a Comment