Monday, May 21, 2012

FLAVIANA MATATA ATOA MSAADA KUMBUKUMBU ZA MV BUKOBA
Mwanamitindo wa kimataifa Flaviana Matata Amekuja nchini akitokea nchini Marekani ambako ndiko yaliko makazi yake  kwa sasa mahsusi kwa ya ajili ya kugawa msaada wa VIFAA VYA KUOKOLEA  MAISHA MAJINI (life vest)  ikiwa ni miaka 16 tangu meli ya MV BUKOBA izame ambapo mama yake mzazi alifariki kwenye ajali hiyo anatarajia kugawa msaada wa vifaa hivyo  Jumatatu ya 21 May  jijini mwanza.

Flaviana Matata akikabidhi msaada wa maboya 500 kwa mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Elias Makori kulia ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba, anayeshuhudia ni Meneja Masoko na Biashara wa Shirika la usafirishaji wa majini mkoani Mwanza la Marine Service,Kapten Obadia Nkongoki. Igoma jijini Mwanza,
Flaviana Matata akishindwa kujizuia na kuangua kilio wakati wa ibaada ya kumbukumbu ya miaka 16 ya ajari ya meli ya MV Bukoba alipotembelea baadhi ya makaburi ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo yaliyopi Igoma jijini Mwanza, katika ajali hiyo Flaviana alimpoteza pia mama yake mzazi.
Waombolezaji wengine waliofiwa na ndugu zao wakiombea marehemu wa ajali hiyo
Flaviana akionesha moja ya maboya yenye nembo ya foundation yake aliyokabidhi katika kumbukumbu ya miaka 16 ya ajali ya MV Bukoba ikiwa ni kampeni yake ya kupunguza ajari za majini hapa nchini.
Flaviana na wageni wakiweka  mashada kwenye makaburi ya waliofariki kwenye ajali hiyo Igoma Mwanza

1 comment: