MDHAMINI WA MASHINDANO YA MKWAWA MAGIC SITE NGD STEVEN NYANDONGO
Hitimisho la mashindano yaliyokuwa yakiendeshwa katika Manispaa ya Iringa yamemalizika
leo. Mashindano hayo yalijumuisha timu katika mitaa yote ya Manispaa ya
Iringa. Akieleza mdhamini wa mashindano hayo Ndg. Steven Nyandongo Mkurugenzi wa kituo cha Utalii Mkwawa Magic Site alisema nia ya mashindano hayo ni kuwapa changamoto vijana katika mchezo wa mpira wa miguu na kuwafanya wajitume kimazoezi zaidi ili hapo baadaye tuweze kupata wachezaji watakaosababisha Ligi Kuu ichezwe hapa kwetu Iringa.
Akielezea gharama za ujumla katika michezo hiyo ni shilingi milioni tatu ambazo zimegawanywa kwa matumizi yafuatayo:
§ Posho kwa Waamuzi
§ Viburudisho kama vile maji, soda n.k
§ Zawadi kwa timu zote zilizoshiriki mashindano haya na kila timu ilipata mpira mmoja mmoja.
Zawadi ya mfungaji bora aliyepata seti ya viatu vya mpira kutoka Timu ya Viziwi ya Mtwivila.
Zawadi kwa Golikipa bora aliyepata seti ya jezi moja.
Ngao kwa timu yenye nidhamu ilichukuliwa na Timu ya Viziwi ya Mtwivila
Zawadi kwa washindi wa pili ambao walipata Kikombe, mpira na mbuzi mmoja Timu ya Zizi la Ng’ombe
Zawadi kwa mshindi wa kwanza aliyepata Kikombe, mpira, seti ya jezi pamoja na mbuzi mmoja nao ni Timu ya Mashine tatu.
Akitoa shukrani Katibu wa Chama cha mpira wa miguu Iringa Ndg. Eliud Mvela aliomba mashindano haya yawe yanafanyika kila mwaka na wao kama chama watashiriki kusaidia namna ya uendeshaji.
|
No comments:
Post a Comment