Sunday, May 20, 2012

MISS EAST AFRICA 2012 -UGANDA

Miss Ayisha Nagudi kutoka Uganda

Washiriki watakaoziwakilisha Nchi zao katika fainali mashindano ya Miss East Africa 2012 wanaendelea kutangazwa katika mchujo ulioendeshwa na kampuni ya East Africa gazelle ya Nchini Uganda.
Mrembo aliyetangazwa mwishoni mwa wiki ni  Miss Ayisha Nagudi (23)  kutoka Nchini Uganda atakayeiwakilisha Nchi hiyo katika fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012.
Miss Ayisha Nagudi  ana urefu wa 1.82m ni mwanafunzi wa mwaka pili katika chuo kikuu cha Makelele jijini Kampala, ambapo anasomea degree ya Education
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 ambazo huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.

No comments:

Post a Comment