Sunday, May 13, 2012

KIKULA SPORT BONANZA LA MALIZIKA JANA UDOM

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula alipokua akifungua bonanza hilo ambapo ilikua ni siku ya mwisho ya fainali ambapo karibia michezo yote ilikua ikikutana kwenye fainali.
Timu za Mpira wa Miguu Kutoka Vitivo Vya Sayansi ya Jamii na Kutoka Kitivo Cha Elimu Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa mbele ya jukwaa la mgeni rasmi Prof Idris Kikula Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)(Hayupo Pichani).Kutoka Kushoto Wenye Jezi za Blue Ni Timu kutoka Kitivo Cha Elimu na Mwenye Jezi za Orange ni timu ya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii Zote Kutoka UDOM
Timu zote za Michezo Wa Mpira wa Miguu, Kikapu, Nyavu za Vitivo Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma zilizoingia fainali katika bonanza la KIKULA SPORT DAY BONANZA linalofanyika kila mwaka huku mwaka huu ukiwa ni mwaka wa pili tokea kuanzishwa kwake.

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula Kisalimiana Na Wachezaji Wa Timu ya Mpira wa MIguu kutoka Kitivo Cha sayansi Ya Jamii kabla ya Mchezo wao Wa Fainali na Timu ya Kitivo Cha Elimu
Mchezo wa Mpira Wa Miguu Ukiendelea Hadi Kufikia Mwisho Hakuna Aliyeona Nyavu Za Mwenzake na Ref kuamua timu zote kwenda kwenye matuta
Mchezaji wa Timu ya Kitivo Cha Elimu Edward Mzelu alipopiga Penati ya Mwisho Na Kuipa Ushindi wa Magoli 5 kwa 4 dhidi ya Timu ya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii na Kitivo Cha elimu Kuibuka Washindi wa Mashindano ya Kikula Sports Day Bonanza

Mashabiki pamoja na wachezaji wa kitivo cha elimu wakishangilia mara baada ya kuibuka washindi kwa kuifunga kitivo cha sayansi ya jamii kwa mikwaju ya oenati 5 kwa 4

 Mchezo wa Netball Kati ya Kitivo Cha Elimu Na Kitivo cha Sanaa na Lugha ukiendelea na Kitivo Cha  Elimu kuibuka washindi
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula Akisalimiana na Wachezaji wa Mpira wa Kikapu Kabla ya MChezo huo Kuanza
Add caption
Mechi kati ya Kitivo cha Elimu na Kitivo cha Sayansi ya Jamii ukiendelea na Kitio cha sayansi ya jamii kiibuka mshindi katika mechi hiyo
 
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula Akifuatilia Mchezo wa Volleybal Wakati wa Mechi dhidi ya Kitivo Cha Sayansi ya Jamii na Kitivo Cha Elimu hapo jana katika bonanza lililoshirikisha wafanyakazi pamoja na wanafunzi
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula akiongea na Waandishi wa Habari wakati wa bonanza la Kikula Sports Day likiendelea hapo jana katika viwanja vya michezo vya Chuo Kikuu Cha Dodoma vilivyopo Katika Kitivo Cha Sayansi ya Jamii.

Wadada waliojitokeza Kwenye Shindano la Kula katika bonanza hilo lililofanyika jana katika viwanja vya kitivo Cha Sayansi ya Jamii.
Washiriki wa Shindano la Kula Hao wakiendelea kushindana Kula katika Bonanza la Kikula Sports Day lililofanyika Jana katika Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma
Zoezi la Ushindani Wa Kula likiendelea hapo
Mshindi wa Shindano la Kula aliyeshikwa mkono akionyeshwa kuwa ndie mshindi wa kula katika bonanza hilo lililofanyika jana katika viwanja vya chuo kikuu cha Dodoma ambapo lilidhaminiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof Idris Kikula pamoja na Kampuni ya Vinywaji Ya Coca Cola
Prof Idris Kikula (Katikati) akitabasamu wakati mchezo wa kukimbiza kuku kwa wafanyakazi ukiendelea katika bonanza lililofanyika jana Katika viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Meneja Wa Kampuni Ya Coca Cola Kanda ya Kati Dodoma Bwana Maginga Akitoa Shukrani ka Uongozi Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Na Vilevile Ndio KAmpuni iliyodhamini bonanza hilo Na Hapo alikua akikabidhi Zawadi Za Kreti za Soda kwa Uongozi Wa Chuo Kwaajili ya Kukabidhi kwa Washindi Wa Michezo Mbalimbali
Msanii Chipukizi Chipoka akitoa burudani katika bonanza hilo lililofanyika jana katika Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)

Tukibadilishana Mawazo na Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)Prof Idris Kikula (Wa pili Kulia), Wa Kwanza Kulia Bwana Josephat Lukaza, Wa Kwanza Kushoto Ni Kijana Abdul na Wa pili Kushoto Ni Mkuu wa Masomo ya Shahada ya Kwanza Prof Msofe tulipokutana Jana Katika Bonanza La Kikula Sports Day

Baadhi ya Wanafunzi Waliojitokeza Kutazama na Kushuhudia Bonanza Hilo lililofanyika Jana Katika Viwanja Vya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) ambapo bonanza hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Coca Cola pamoja na Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula

No comments:

Post a Comment