Sunday, May 13, 2012

BREAKING NEWSSS,,,,,, UCHAGUZI WA WANAFUZI WASITISHWA RUCO

Uchaguzi wa serikali ya wanafunzi wasitishwa RUHAA UNIVERSITY COLLEGE kutokana na siasa ya CCM na CHADEMA kutawala chuoni hapo, Hali inayo pelekea kutokuwepo kwa dalili ya amani na utulivu kama kampeni za  uchaguzi huo zikiendelea,,, ripoti zaidi na mwanafunzi mwenzetu kutoka chuoni hapo,,,
RUHAA UNIVERSITY COLLEGE, IRINGA, TANZANIA
"Katika hali isio kuwa ya kawaida wanafunzi wa chuo kikuu cha Ruhaa walijikuta wakipigwa na butwaa baada ya mkuu wa mkoa wa Iringa kutangaza kusimamishwa kwa harakati za uchaguzi chuoni hapo kwa sababu ya kutawala kwa siasa za CCM na CHADEMA,
Aidha mkuu wa wa mkoa wa Iringa imembidi kufanya hivyo kutokana na kutawala kwa uchadema kwa wagombea wa uongozi chuoni hapa, hali ambayo jana wanafunzi wali funga geti na kuzuia gari lililokuwa linatakakuingia chuoni hapo kutokana na kuwa na bendera ya CCM pamoja na watu waliovaa sare za CCM,
Wanafunzi  wanaojiita wanachadema walikuwa wakitaka watu walio kuwamo ndani ya gari hilo watoe maelezo wanakuja chuoni hapo kufanya nini ndipo waruhusiwe kupita. Hata hivyo wanafunzi hao hawakuliruhusu gari hilo kuingia chuoni hapo.
Taarifa zilizo tufikia hivi punde Mkuu wa chuo ametangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi ni 16 may lakin hadi hivi sasa hakuna hakujabandikwa majina ya wagombea uchaguzi huo,,,, "

No comments:

Post a Comment