Tuesday, May 15, 2012

MALALAMIKO KUTOKA KWA WANAFUNZI KWA TCU

ADHA YA MFUMO WA MALIPO TCU ZAITAJI KUTATULIWA,,,,
 Kutoka kwa mdau,,,,,,,
Nina mdogo wa rafiki yangu ambaye ni mhitimu wa form six ambaye alikuwa ana-apply kwa ajili ya kupata nafasi chuo kikuu na na pia kupata mkopo. Feedback niliyoipata kutoka kwake kwa ufupi sana ni kama ifuatavyo: 

  • Ni mfumo wa kisasa kabisa unaotumika kufanya hizo applications. Sijali kama umetengenezwa nje au tumetengeneza wenyewe. Either way, Big Kudos kwa TCU.
  • Ubunifu wa kutumia voucher nao ni "mzuri" kwenye ku-create user account kwa yule anaye-apply na kwenye kukusanya malipo. Kwa sababu zisizo very clear kwangu inaonekana kama inahitaji ka-kosa kadogo sana kwa mtu kujikuta voucher yake inakuwa "invalidated au locked out" na kwa hiyo kulazimika kutoa 30,000/= nyingine ili kuendelea na hiyo application. Kwa kutambua hali ngumu za kipato cha watanzania kwa nini hapa kusiwe na uvumilivu zaidi ya ilivyo sasa. Nammanisha kwa nini system isimpe mtu nafasi ya kufanya makosa say kwa standard za kawaida za "kibenki" kuwa unakuwa locked out baada ya 3 unsuccesifull entries? I'm led to believe (correct me if i'm wrong) kuwa kwa mfumo wa sasa KOSA MOJA, GOLI MOJA (30,000 THS, GONE!).Hii naona ni a very big weakness!
  • Kuwa kuna applications zinazo-run tu kwenye browser ya Firefox. Kwa kujua kuwa most people wanatumia other browsers (Internet Explorer ikiwa ndo the most popular) kwa nini option ya IE kwa mfano isiwepo.
Ninatambua juhudi kubwa ambazo zimewekwa na TCU kuweza kutufikisha hapa. Kama kuna mtu anweza kuyafikisha maswali haya na pongezi hizi kwa TCU moyo wangu na mingine mingi naamini itakuwa imepata faraja hata kama itakuwa ni ya muda!
-- 

Wasalaam
Denis Matanda,
Mine Supt,
Nzega - Tanzania.

Comments kutoka kwa wadau.
Tatizo sio kukosea ila kadi zao za malipo zina tatizo ambalo hawataki kulitangaza. Nimekutana na adha kama yako na kwa sababu niko Dar es Salaam niliamua kwenda ofisini kwao kuulizia, nilizuiwa na mlinzi wa getini na akaniambia nimueleza naenda kufanya nini. Nilisikitika kwa sababu mimi nilikuwa nataka kwenda mapokezi niombe wahusika wanifafanulie ni kwanini, nilipo mueleza mlinzi akaniambia amepewa maagizo kwamba watu wenye shida kama hii ni wale wenye kadi zilizo andikwa 50,000 lakini zinauzwa 30,000, hii ni kutokana na kwamba kuna kitu walikuwa wanazifanyia kwenye mfumo na baada ya masaa matatu zinge anza kukubali, ajabu ni kwamba baada ya hayo masaa matatu nimekuwa nikjaribu bila mafanikio.
Ushauri kwa TCU ukianzisha huduma kama hii unahitaji line zaidi ya moja za simu kuhudumia wateja kwani sio kila mtu anaweza kufika ofisini kwenu na vile vile nasikia mna maenyesho ya namna ya kujisajili kwenye viwanja vya chuo kikuu cha DSM kijitonyama, je watu wa mikoani mnatufikiria vipi? Na mlichukuaje uamuzi kutmia benki ya NBC kuuza hizi kadi wakati hawajasambaa Tanzania nzima kama ilivyo NMB au ofisi za Posta? Je mnahudumia watu wa mijini tuu?


2 comments:

  1. Karume Institute of Science and technology kilichopo Mbweni,Zanzibar wamesajili wanafunzi kinyume na sheria(wamesajili wanafunzi wasiotambulika TCU) ,kuanza degree wamekula ada zao mwaka mzima na kuwaondosha kimyakimya bila kurudisha ada zao .Wamezuia matokeo nisiyaone na kunitishia kuniharibia CV yangu .TCU amkeni Taifa linawaamini kusaidia wanafunzi.

    ReplyDelete