Na.Mwandishi wetu
Mrembo
anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2011/2012 Nelly Kamwelu
kwa kushirikiana na Mfuko wa Saratani ya Matiti Tanzania (Breast Cancer
Foundation) leo atafanya harambee ya kuchangia mfuko wa saratani ya
matiti itakayofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Harambee
hiyo imepangwa kuanza saa 1.00 usiku kwa mujibu wa muandaaji wa
mashindano ya Miss Universe Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni
ya Compass Commutations, Maria Sarungi Tsehai.
Maria
alisema kuwa katika hafla hiyo kutakuwa na mnada wa kito cha Tanzanite
ambayo imetolewa maalum na kampuni ya Richland Resources kwa ajili ya
kuchangia mfuko huu. Pia picha ya Mrembo wa Miss Universe Tanzania
itanadiwa katika mnada huo.
Mrembo
Nelly Kamwelu toka achukue taji la Miss Universe Tanzania 2011, amekuwa
akifanya kazi bega kwa bega na mfuko wa saratani ya matiti ikiwamo
kusaidia kutoa elimu katika shule mbalimbali ili kupunguza au kutokomeza
uwezekano wa kuenea kwa saratani ya matiti. Mfuko huu umepanga
kuendeleza elimu hii kwa shule za mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Iringa,
Mtwara na Lindi.
Kwa
kusindikiza hafla hii kutakuwa na maonyesho ya mavazi yaliyotolewa na
wabunifu wa hapahapa nchini ambao ni Escado Bird, Kemi Kalikawe na
Subira Wahure vilevile kutakuwa na burudani ya muziki kutoka msanii
Enika na mchekeshaji Evans Bukuku. Pia mrembo mwenyewe Nelly Kamwelu
atatoa burudani ya dansi aina ya Belly Dance.
No comments:
Post a Comment