Friday, May 18, 2012

WENGI WAJITOKEZA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MCHEZAJI WA SIMBA, MAREHEMU PATRICK MAFISANGO


 Mchungaji akiendesha ibada maalumu ya kuuaga mwili wa marehemu Mafisango
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba, marehemu Patrick Mafisango, tayari kutolewa heshima za mwisho leo kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam
Msafara wa mwili wa Mafisango ukiongozwa na Trafiki, kuingia viwanja vya TCC Chang'ombe, Dar es Salaam leo
Sehemu ya umati wa waombolezaji waliofika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa  marehemu Mafisano. Picha na Dotto Mwaibale.

Waziri wa  Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta akilia kwa uchungu baada ya kuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa kimataifa wa Klabu ya Simba Patrick Mafisango.

Tulikupenda sana Kampumzike kwa Amani.

Mchezaji wa Simba Haruna Moshi a.k.a Boban akiwa haamini macho yake baada ya kuutazama mwili wa mchezaji mwenzake. Aliyemshikilia ni Mwenyekiti wa Simba SC Ismail Aden Rage.

Juma Kaseja akilia kwa uchungu.

Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi akiaga.

Wachezaji wa timu ya Taifa “Taifa Stars” wakitoa heshima za mwisho.

“Kwa heri Mafisango”

Mashabiki wakilia kwa uchungu.Kikosi cha Redcross wakitoa huduma ya kwanza.

1 comment: