Thursday, May 24, 2012

ELIMU NA VIJIMAMBO IFM

Mmoja wa wanafunzi wa IFM akijisomea usiku
"Katika hali ya kushangaza Siku ya jana subuhi ya Jumatano hapa ifm kumetokea tukio la kushangaza sana baada ya mtihani kuahirishwa huku watu wakiwa katika venue za mitihani,tukio hilo la kushangaza liliwakumba member wote wa mwaka wa pili wanaosoma somo la hesabu,
Wahanga hao walikuwa ni wa course zifuatazo yaani computer science,information technology,insurance,banking and finance,accounting na social protection,
Tukio hilo liliwakuta watu wakiwa tayari wameshajiandaa kufanya mtihani huo huku wakiwa na morali wa hali ya juu,
Hata hivyo sababu za kuhairishwa kwa mtihani huo hazikufahamika kwani wahusika wenyewe hawakuwa tayari kuongelea suala hilo,ila baada ya wadau kuhangaika hapa na pale ilikuja kubainika kuwa mtihani huo ulivuja yaani asilimia kubwa ya candidates wa huo mtihani waliupata mtihani huo mapema mida ya saa kumi alfajiri na kwa maana hiyo watu walisolve gaka,
Sasa haijulikani ni nani aliyevujisha huo mtihani kwani kama aliyevujisha huo mtihani ni mwalimu husika kwanini ahairishe mtihani?
Ama hakika sijui elimu yetu ya Tanzania ni wapi inaelekea kwani hadi mitihani ya test inavujishwa je final exam itakuwaje? 
Wakati huo huo tukio hilo limewaweka watu katika mashaka ya kuhudhulia tukio la miss ifm litakalofanyika hapo siku ya ijumaa katika ukumbi wa blue pearl maeneo ya ubungo, kwani inasemekana mtihani huo utafanyika tena siku ya jumamosi, hivo kwa wale watakaoudhuria sherehe hizo watakosa muda wa kujiandaa., Poleni sana wadau ila ndo faida ya kuiba mtihani hiyooooo!!!"

No comments:

Post a Comment