Tuesday, May 8, 2012

IFM-SO FIRST ELECTION RESULTS

Matokeo ya uchaguzi wa serikali ya wanafunzi IFM-SO round ya kwanza uliofanyika jana katika chuo cha biashara IFM yametangazwa na reporter wenu anatuhabarisha zaidi,,,,

"Hayawi hayawi  sasa ya mekuwa,hatimaye primary election ya kamilika  na matokeo ya metoka kutangazwa usiku huu wa saa sita katika viunga vya IFM, kiukweli katika viunga kelele za shamra vifijo na nderemo kutoka kwa wadauu wa ndugu MICHAEL CHARLES na wapinzani wao wa karibu crew la ndugu EMMANUEL KALINDAGA walikuwa wakishangilia kwa furaha sana hata hivyo kwa upande mwingine wa wagombea waliotolewa hali ilikuwa tofaut kidogo kwani walikuwa ni wenye huzuni sanaa.  Niliongea na wadau wawili watatu wa waliotolewa kwenye kinyan'ganyiro hicho na wakadai kuwa katika ushindani lazima apatikane mshindi na hivo wao wametolewa ili mshindi aweze kupatikana kwani bila wao rais asingepatikana.
Ndugu Michael Charles alimuacha mpinzani wake wa karibu kwa kura nyingi sana kura zipatazo takribani 300,
Hata hivyo muamko wa kupiga kura umeonekana kuwa ni mdogo sana kwani chuo kina wanachuo wapatao 7000 na wanachuo waliopiga kura ni asilimia thelathini tu ya kura zote,
kura zilizopigwa ni kura 2096 na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo,kulikuwa na vituo vinne, ambavyo vilipangwa interms of course na matokeo yalikuwa kama hivi:
kituo cha kwanza;
TAX MANAGEMENT
MICHAEL CHARLES 248
EMANUEL KALINDAGA 47

JEREMIAH MAYENGA 192
EMANUEL HEZRONI 63

kituo cha pili;
INSURANCE AND SOCIAL PROTECTION
MICHAEL CHARLES 191
EMANUEL KALINDAGA 303
JEREMIAH MAYENGA 77
EMANUEL HEZRONI 20

kituo cha tatu ;
BANKING AND ACCOUNTING
MICHAEL CHARLES 145
EMANUEL KALINDAGA 73
JEREMIAH MAYENGA 46

EMANUEL HEZRONI 122
Kituo cha nne;
COMPUTER SCIENCE NA INFORMATION TECHNOLOGY
EMANUEL KALINDAGA 88
MICHAEL CHARLES 291
JEREMIAH MAYENGA 80
EMANUEL HEZRON 54,
Na kwa maana hiyo ndugu Michael Charles kajikusanyia kura 875 akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu ndugu Kalindaga mwenye kura 508, na mshindi wa tatu ni mheshimiwa Mayenga mwenye kura 395 na nafasi ya nne imeshikwa na Emanuel Hezroni mwenye kura 259 na kura zilizoharibika ni 16 tu.
Na kwa hali hiyo Mh. Michael na Mh. Kalindaga ndiyo watakaoshindana katika final election itakayofanyika siku ya Ijumaa. Hivi ndivyo ilivyokuwa Jumatatu yetu hapa Ifm, Ni yule yule reporter wenu KITOP at ifm"
habari picha zina kuja hivi punde,,,,,!!!!

No comments:

Post a Comment