Mkurugenzi
wa Project ya Indiafrica Dr. Seema Kundra akifafanua mchakato mzima wa
Indiafrica ( A Shared Future) utakavyokuwa nchini Tanzania.
Mwakilishi
kutoka Ubalozi wa India Kunal Roy (wa kwanza kulia) akielezea sababu za
Ushiriki wa Serikali ya India katika Project ya Indiafrica.
Mbunifu
wa Mavazi kutoka Tanzania Mustafa Hassanali (kushoto) akifafanua
ushiriki wa vijana wadogo wanaochipukia katika nyanja za ubunifu na
jinsi watakavyofaidika kupitia ushirikiano wa Swahili Fashion Week na
Indiafrica.
Mwakilishi
kutoka chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr. Mbura akizungumza jinsi mdahalo
kuhusu Indiafrica utakavyoendeshwa katika Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam.
INDIAFRICA
(A Shared Future) ni mpango wa kimawasiliano unaojumuisha mashindano
mbalimbali kama, uandishi wa insha, upigaji picha na ubunifu. Hii
itasaidia kujenga jukwaa la vijana kutoka Afrika naIndiawenye vipaji na
uwezo wa kushirikiana katika changamoto na mafanikioyao; Na baadae
kushirikiana kiubunifu, biashara na utamaduni.
Kwa
Tanzania mchakato mzima itakuwa tarehe 12 Mei 2012 ukumbi wa Nkuruma
chuo kikuu cha Dar-es-salaam kuanzia saa 2:00 asb-7:00mch awamu ya pili
itakuwa saa 8:00-11:00jioni.
Baada
ya mdahalo jioni wasanii Chid Benzi na Dully Sykes kutoka Tanzania
watatoa burudani kwa washiriki vijana wajasiliamali wenye maono ya
mafanikio na maendeleo. Washindi watapata fursa ya kutembelea Afrika na
India.
No comments:
Post a Comment