Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ikishirikiana na Baraza laTaifa la Elimu ya Ufundi inapenda
kuwataarifu waombaji wa Udahili wa elimu ya juu kwa mwaka 2012/2013
hasa kwa wale wanaotakiwa kuomba kupitia mfumo wa Udahili wa Pamoja kuwa
kwa wale waliomaliza kidato cha sita, Diploma za Elimu Ufundi na ualimu mwaka 2012 wataanza
kutuma maombi yao ya udahili kuanzia tarehe 7 Mei 2012 mpaka tarehe 30
Juni 2012. Waombaji wote wanapaswa kutuma maombi yao katika kipindi hiki
kwa kuwa hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe ya mwisho.
Gharama ya maombi ya udahili kwa mwaka huu ni TSh.30,000 tu (elfu thelathini tu) kwa waombaji wenye vyeti vya mfumo wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Malipo yatafanyika kwa kupewa kadi ambazo zinapatikana kwenye matawi yote ya NBC nchi nzima.
Waombaji wanashauriwa kununua kadi hizo katika matawi ya Benki ya NBC tu na si vinginevyo.
Waombaji wa kundi la Diploma ya Ualimu na Diploma ya Elimu Ufundi (FTC) wanataarifiwa kuanza kutuma maombi yao siku ya Jumatatu tarehe 7 Mei, 2012.
Vilevile: Waombaji wanajulishwa kwamba pamoja na baadhi ya kadi kuwa zimeandikwa Tsh 50,000 malipo ya kadi yataendelea kuwa Tsh. 30,000 tu hata kwa kadi hizo,
NB: Waombaji wote wanashauriwa wazitunze kadi zao vizuri baada ya kuzitumia kwa uthibitisho endapo zitahitajika.
Waombaji ambao si watanzania watatakiwa
kulipa $60 (dola za kimarekani sitini tu) katika matawi ya Benki ya NBC
na watapewa namba ya kutumia mfumo wa Udahili wa Pamoja (CAS) kwa ajili
ya udahili.
Tume pia inawataarifu waombaji wenye vyeti
ambavyo si vya mfumo wa elimu ya Tanzania (mfano. Cambridge,
Baccalaureate, Uganda nk.) kwamba wataanza kuomba udahili kuanzia tarehe
21 Mei 2012 na kwamba vyeti hivyo view vimeshathibitishwa na NECTA.
TAHADHARI:
Wanafunzi
waliomaliza kidato cha sita wasio na ufaulu wa angalau alama ‘E’ mbili
na angalau na alama ‘C’ tatu kidato cha nne wanashauriwa wasiombe
udahili wala kununua kadi kwa kuwa hawana kiwango cha chini
kinachohitajika kwa ajili ya udahili wa kujiunga na kozi za shahada
katika vyuo vya elimu ya juu. Hivyo inashauriwa kusoma sifa
zinazohitajika kwa makini kama zilivyoelezwa kwenye Kitabu cha Mwongozo
wa Udahili ili kuepuka matatizo yanayotokana na kushindwa kufuata
maelekezo.
Imetolewa na ofisi ya Katibu Mtendaji,
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
Tarehe 04/05/2012
No comments:
Post a Comment