Baadhi ya wanachuo wa chuo cha ualimu cha Singida mjini waliohudhuria mahafali ya tano. |
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone akizungumza kwenye kilele cha
mahafali ya tano ya chuo cha walimu mjini Singida. Kulia ni Mkuu wa chuo
hicho cha walimu Didas Monyo.
Mkuu
wa chuo cha walimu cha Singida mjini Didas Monyo akitoa taarifa yake
kwenye mahafali ya tano ya chuo hicho. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida
Dkt. Parseko Kone.
Bango la chuo cha ualimu na shule ya sekondari ya Singida iliyopo mjini Singida. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na.Nathaniel Limu.
Serikali
ya mkoa wa Singida imedai kwamba haina nafasi kabisa ya kupokea walimu
ambao hawana maadili ya ualimu kwa hofu kwamba wanamadhara makubwa
katika ustawi wa sekta ya elimu.
Akizungumza
kwenye mahafali ya tano ya chuo cha ualimu cha Singida mjini, Mkuu wa
mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amesema kupokea walimu ambao hawana
maadili ya ualimu, kuna hasara nyingi tena kubwa, zikiwemo kushusha
taaluma na kuchangia kuharibu maadii ya wanafunzi.
Kuhusu
wahitimu walimu tarajiwa hao 559, Dkt. Kone amesema anafahamu kuwa
watakuwa wamechagua au kuchaguliwa kwenda kufanya kazi ya ualimu katika
mikoa mbali mbali ya Tanzania , ikiwemo mkoa wa SIngida.
Awali
mkuu wa chuo cha ualimu Singida Didas Monyo, alitaja changamoto mbali
mbali zinazokikabili chuo hicho, kuwa ni pamoja na upungufu wa vitabu
vya kufundishia (kiada) na uhaba mkubwa wa maji.
Kwa
mujibu wa mwalimu Monyo chuo hicho kina wanahcuo 1,610, kati yao wapo
wa mwaka wa kwanza 1051 na wa mwaka wa pili ambao ndio wahitimu ni 559.
No comments:
Post a Comment