Thursday, May 3, 2012

VIJIMAMBO VYA UCHAGUZI IFM, LEO

JANA USIKU
KITOP, repoter ifm.
Mgombea  urais wa wanafunzi katika chuo cha  IFM afumwa Kigamboni kwenye magetto ya masela akipiga kampeni. Bila ya kumuangusha mgombea huyo wanafunzi walizindi kumsupport na kumhakikishia ushindi repoter wetu anasema
"Duuhu  kweli hii kali, jamaa alichokuwa anafanya ni kupita kila nyumba ambayo wanachuo wa IFM wanaishi alipita yeye na timu yake ya watu kama kumi hivi na alikuwa akiomba kura,alichukua namba za cm za watu wote aliokuwa akiwatembelea,"
Baada ya mgombea huyo kuondoka kama kawaida ya wanafunzi walianza kujadili na kuibuka na maswali kama yafuatayo
"watu wanajiuliza hivi ni sahihi kwa mujibu ewa sheria za chuo kampeni hazi na muda wa kikomo?"
"Jamaa ataendelea na moyo huu akipata nafasi, (yaani kutembelea watu ghetto)?"
Japo kuwa maswali hayo yalimfikia mgombea na hakuweza kuyatolea ufafanuzi wakutosha kwa wanafunzi walio muuliza maswali hayo, ila mgombea huyo aliendeleza kampeni zake za usiku nyumba hadi nyumba hakujali ni usiku wa sangapi wala atakua anawafanyia watu fujo.
Aidha timu hiyo ya watu zaidi ya kumi ikiendelea kufanya kampeni za usiku kwa usiku zenye jina maarufu kama " ushindi daima" zilifika kikomo saa nane na nusu za usiku  na kuelekea kivukoni ambapo walikosa usafiri wakuwavusha kurejea chuona na hivyo kuwa lazimu walale Kigamboni station.
MCHANA WA LEO 
Harakati za kampeni zikiendelea chuoni IFM leo mchana kumekuwa na msongamano mkuwa wa vuta nikuvute kati ya wagombea kiti cha urais, MICHAEL CHARLES mgombea urais alionekana kuwavutia watu wengi wakiwemo wasichana repoter wetu na haya ya kusema


"mademu wana mkubali sana  "MICHAEL CHARLES" niliongea na wasichana kama nane hv wa course tofaut ambao walikuwa wamekaa kwenye vimbweta vya chuo hapa, nikawauliza hivi ni nani mnahisi anaweza akaachiwa nafasi warembo hao wa course tofauti zikiwamo BANKING,TAX ADMINISTRATION NA SOCIAL PROTECTION waliongea bila kuficha na kusema watafurahi kama ndugu MICHAEL atakuwa presidaa",

Sababu zinazo semwa na wengi za kumpa ushindi wa kishindo MICHAEL zilielelwa na repoter wetu
 "Ni lipo kuwa na zunguka huku na kule na sikia jina la MICHAEL lina tajwa kwa wingi hapa chuoni ndipo nilipo anza kuwauliza wanafunzi tofauti tofauti na wakigoma kujitambulisha kwa majina ile swali langu lilikuwa ni hili hapa 'Kwa nini una taka MICHAEL awe raisi wako' sababu zilikuwa nyingi sana ila zilizo jirudia kwa wingi ni hizi hapa

1.kwanza jamaa ni mtanashati/handsome. 'walisema ma binti wengi chuoni hapa'
2.sera zake ni nzuri na anajiamini yaani hana uoga. 'baadhi ya wavulana walisema '
"

UFISADI WA IFMSO 
Kumbe  hata viongozi wa wanafunzi ni mafisadi, kweli Tanzania tutafika, katika harakati za kampeni wagombea walijikuta wakiropoka mabaya  yaliokuwa yakifamwa na viongozi wa serikali ya wanafunzi iliyopita IFMSO, repoter wetu anahabari kamili
"Katika hali isiyokuwa ya kawaida wanachuo wa IFM walionekana wakifurahia siri zilizokuwa zikifichuliwa na wagombea wa urais kuhusu mabaya yaliyokuwa yakifanywa na serikali iiyopita, kuna vitu vingi vilivyokuwa vimetokea ikiwamo pamoja na ufujaji wa pesa uliofanywa na viongozi hao wa IFMSO waliopita,maneno hayo yalisemwa na mmoja wa wagombea hao ambaye jina lake limehifadhiwa mgombea huyo alisema
"pesa za wanachuo zimetumika vibaya hasa katika siku ya carrier day iliyofanyika trh 28 mwezi uliopita kwani matumizi ya kuandalia sherehe hiyo yalikuwa ni madogo ukicompare na bajet waliyoiandaa na kuifikisha kwenye kikao cha bunge" 
vile vile fedha za mfuko wa IFMSO ilikuwa ni milioni 24 na siyo milioni 17 kama walivyotangaza wao viongozi wa awamu iliyopita,ubadhilifu huu wa pesa za serikali ya IFMSO Inabidi ukemewe ipasavyo kwani unarudisha nyuma maendeleo ya nchi. alimalizia kwa kusema
amahakika hii nchi sijui inaenda wapi kwani ufisadi umejaa kila mahal.
MUNGU IBARIKI IFM MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU IBARIKI AFRIKA KWA UJUMLA. "
 

No comments:

Post a Comment