Wednesday, May 2, 2012

SHINDANO LA INSHA AU MICHORO, HAKI ELIMU.

Shindano la insha na michoro la HakiElimu
HakiElimu kwa kushirikiana na jukwaa la katiba Tanzania, leo imezindua shindano la insha kuhusu mchakato wa uandikaji katiba mpya, mada inayoshindaniwa ni 'Katiba mpya iseme nini kuhusu elimu?'.
katika uzinduzi huo, mwenyekiti wa jukwaa la katiba Bw Deus Kibamba aliwaomba watanzania kutoa mawazo yao juu ya nini wanataka kijumuishwe kwenye katiba mpya kuhusu elimu kwa kufafanua kwamba katiba ya sasa inaiongelea elimu kama ni haki ambayo watanzania hawawezi kuidai.


"Katiba ya sasa inatoa fulsa ya kuwa kila mtanzania ana haki ya elimu kwa kujitafutia yeye mwenyewe", alisema Kibamba akifafanua kuwa katika mazingira hayo mtanzania hawezi kuidai haki hiyo mahali popote.

Mwisho wa kupokea insha au michoro ni tarehe 30 Juni 2012 ambapo washindi watatangazwa mwezi septemba.

Izingatiwe kuwa washindi tuu ndo watakaotangazwa.

No comments:

Post a Comment