Friday, June 8, 2012

ZANZIBAR HEROES YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA DUNIA

Wachezaji wa Zanzibar Heroes

TIMU ya soka ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa nchi zisizo wanachama wa FIFA, VIVA World Cup, baada ya kuifunga Tamil Elaam mabao 3-0 katika mchezo wa Kundi B, uliofanyika usiku wa jana mjini Erbil, Kurdistan.
Katika mchezo huo, mabao ya Zanzibar Heroes yalitiwa kimiani na Hamisi Mcha dakika ya 22, Amir Hamad dakika ya 61 na Awadh Juma dakika ya 90.
Kwa matokeo hayo, Zanzibar itacheza na Cyprus katika Nusu Fainali kesho saa 3:00 usiku Uwanja wa Suleimaniya, nje kidogo ya mji wa Erbil.

No comments:

Post a Comment