Sunday, June 3, 2012

JE IFM INAONGOZWA NA FREEMASON,,,,?

Katika hali ya kushangaza ndani ya Institute of Finance Management  (IFM)  wikend hii kumetokea maamuzi ya ajabu kutoka katika management ya chuo. Na kupelekea wanafunzi wa chuoni hapo kuwa na wasiwasi na utawala wa chuo hicho kuwa kinawezekana kina ongozwa na FREEMASON, Habari zaid na mwanaharakati wetu,,,,
KITOP at ifm
"Watu wameanza kuhisi tofauti na kuhofia labda IFM inaongozwa kwa nguvu za freemason, Kutokana na maamuzi ya utawala wa chuo yalio tangazwa wikend hii kuzuiya wanafunzi wote kufanya shughuli zao za kidini maeneo ya chuo hapa.Taarifa hiyo imetolewa na utawala ikisema  wamezuia watu kusali katika lecture rooms na maeneo yanayozunguka IFM kwa madai kuwa eneo la ifm ni dogo sana hivo inakuwa ni tatizo sana kwa shughuli za kimaso kuendelea mida hiyo ambayo ibada zinaendelea, hata hivyo wanachuo wamekuja juu na kudai sababu zilizotolewa na uongozi huo ni za kijinga na hazina maana kwani wao huwa awafanyi ibada madarasani huwa wanaendesha ibada zao nyuma ya BLOCK C na juu ya block c floor ya nne hivo hawaleti usumbufu wowote kwa wanaosongoka pia wakaendelea kusisitiza hapa ifm watu wamekuwa wakisali miaka yote toka hiki chuo kianze iweje leo ndio muone usumbufu??, 
Baadhi ya viongozi wa kidini walidai hawataacha kusali na wataendelea na shughuli zingine za kidini kama kawaida na hakuna wakuwazuia sio principle wala kiongozi yeyote yule. Viongozi hao walidai kuwa kusali ni haki yao ya msingi na wanaweza kufungua kesi mahakamani kama chuo kitaendelea kushikilia msimamo wao huo. Hata hivyo tatizo hili limewaathiri zaidi wanachuo wote wa jumuiya ya kikristu tu kwani wanachuo wote a jumuiya ya kiislam wana eneo la kuswalia ambalo lipo mita chache kutoka chuoni hapo msikiti huo unapatikana ndani ya hospitali ya ocean road. 
Aidha hadi kufika sasa hatujapata kuongea na uongozi wa chuo kujua ni jinsi gani sheria hii itafuatwa bila kuwaathiri wanafunzi wenye uokovu."
Ni mimi The reporter KITOP at ifm.

No comments:

Post a Comment