Wananchi
wakiwemo Watanzania walikusanyika katika viwanja vya Down Town
Washington DC siku ya Jumamosi June,2,2012 katika kuitikia wito wa
kuunga mkono wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa saratani ya
maziwa, utafiti na elimu dhidi ya ugonjwa huo.
Tukio hili lilianza kwa matembezi ya vikundi vya mataifa mbali mbali wanaoishi nchini Marekani.
Watembeaji
wengi waliohudhuria katika matembizi hayo kutoka majimbo mbali mbali
nchini Marekani. Maradhi ya saratani ya maziwa yanakisiwa kuwadhuru watu
25 milioni kote ulimwenguni ambapo kama hatua haitochukuliwa inakisiwa
watu milioni 10 kufa katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Kina
dada wakiwa katika matembezi ya kupiga vita ogonjwa wa saratani ya
maziwa siku ya Jumamosi June, 2, 2012 ndani ya Washington D.C nchini
Marekani.
Rais
wa Jumuia ya waTanzania DMV Mh. Iddi Sandaly, wa kwanza
kushoto, Waheeda Margaret Gathesha, Chief wa swahilivilla Abou Shatry,
Aunt Rehema, pamoja na Salma Jay Jay pia alikuwepo katika matembezi ya
kupigana na ugonjwa wa saratani ya maziwa Washington DC.
Wazawa
wa Kitanzania wanaoishi nchini marekani wakiwa katika matembezi ya
kupiga vita ugonjwa wa saratani ya maziwa mapema ndani ya Washington D.C
nchini Marekani.
Warembo wa kiTanzania wakiwa mstari wa mbele katika mpango mzima wa kutimiza mwendo wa mile tatu.
Team
Tanzania wakipata picha ya pamoja katika kuitikia wito wa kuunga mkono
wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa saratani ya maziwa, utafiti
na elimu dhidi ya ugonjwa huo.
Mamia
ya watu kutoka sehemu mbali mbali waliungana kwa pamoja katika zowezi
hilo la kuunga mkono wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa Saratani
ya maziwa.
Wananchi wakiwa katika mwendo wa Susan G.Komen. kumaliza vita dhidi ya maradhi ya Saratani ya Maziwa Susan G.Komen. 2012!
Kina
kaka nao pia hawajajiweka nyuma kuunga mkono Susan G.Komen. kumaliza
vita dhidi ya maradhi ya Saratani ya Maziwa Susan G.Komen. 2012! ndani
ya Washington DC.
Ahsanteni
sana Auntie Rehema na Dada Zuhura, kwa kutupa muamko wa kuwajibila na
kushiriki katia zowezi haya hili la kupiga vita ugonjoa huu wa satarani
ya maziwa. M/mungu akujalie Afya njeema Insha-Allah Ameen.!
Team Tanzania baada ya kumaliza matembezi ya Susan G.Komen. dhidi ya kupiga vita maradhi ya Saratani ya maziwa.
No comments:
Post a Comment