Friday, June 8, 2012

MWANAFUNZI AUAWA KWA BOMU NA WENGINE WANNE KUJERUHIWA MKOANI KIGOMA

MTOTO OBEDI MANASE (8) MAREHEMU ALIYELIPUKIWA NA BOMU PICHA NA PARDON MBWATE WA JESHI LA POLISI KIGOMA

Na Mohammed Mhina na Pardon Mbwate-Jeshi la Polisi
Mwanafunzi mmoja wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kigadye wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Abeid Manase(8), amefariki dunia hapo hapo na wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ya kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono walilokuwa wakilichezea.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP Fraisser Kashai, amewataja watoto waliojeruhiwa na bomu hilo kuwa ni wanafunzi wawili wa darasa la kwanza Tuju Seluke(7) aliyejeruhiwa tumboni na Sarah Manase(6) aliyejeruhiwa kwenye paja na mguu kulia. wote wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kigadye wilayani Kasulu.

Kamanda huyo amewata wengine waliojeruhiwa kuwa ni watoto wadogo wenye umri wa miaka minne kila mmoja ambao walikuwa wakichezea bomu hilo kwa pamoja ambao ni Enjord Seluke aliyejeruhiwa kwenye sikio la upande wa kushoto na Isaka Yohana aliyejeruhiwa kwenye jicho la upande wa kushoto.

Kamanda Kashai amesema majeruhi hao wote wamelazwa katika hospitali ya Misheni iliyopo katika kijiji cha Shunge wilauani Kasulu kwa matibabu zaidi na hali zao zimeelezwa kuwa zinaendelea vizuri.

Kamanda Kashai amesema jana majira ya saa 11.00 jioni, huko katika kijiji cha Kigadye, watoto hao walikuwa wakilichezea bomu hilo la kutupa kwa mkono na ndipo lilipowalipukia na kumuua mwenzao na wengine hao wane wakajeruhiwa.

Bomu hilo lilikuwa limefichwa katika moja ya bustani nyumbani kwa Bw. Ayoub James Luvahovi mkazi wa kijiji cha Kidae na likimbia mara baada ya tukio hilo na Polisi wanamsaka.
Katika tukio linguine Kamanda Kashai amesema huko Kasulu, watu wenye silahawamemjeruhi kwa kumpiga risasi tumboni mfanyabiashara mmoja Bi. Deothera Malusha(23) na baadaye kumpora shilingi 150,000 pamoja na simu yake ya mkononi aina ya Nokia yenye thamani ya shilingi 55,000.

Amesema baada ya uporaji huwo, majambazi hayo yalikimbia na kutokomea katika msituni na majeruhi amelazwa kwenye Hospitali ya wilaya ya kasulu mkoni Kigoma na hali yake bado sio nzuri.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia watuhamiaji haramu 52 kwa makosa ya kuingia na kuishi nchini bila ya kibali. 

 
Kamanda Kashai amesema kuwa wayuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo mbalimbali walipokuwa wakifanya shughuli za uvuvi mkoani humo

No comments:

Post a Comment