Sunday, June 24, 2012

KESI YA MWANAFUNZI WA TEKU ALIYEUAWA NA POLISI KUANZA KUSIKIKA MAHAKAMA KUU HIVI KARIBUNI - MBEYA


 Baadhi ya majeraha yaliyotokana na kipigo kwenye mwili wa marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye alikuwa mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU),Mbeya aliyeuawa na Askari wa Jeshi la Polisi mkoani hapa tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].
******
Habari na Mwansidhi wetu,Mbeya.
Kesi ya mwanafunzi anayedaiwa kuuawa na Polisi Mkoani Mbeya,itaanza kusikika Juni 27 mwaka huu katika Mahakama Kuu,jijini Mbeya.

Mwanachuo huyo anayedaiwa kuuawa na Polisi marehemu Daniel Mwakyusa,aliyekuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) kilichopo jijini hapa,tukio lililotokea Februari 14 mwaka huu.

Imedaiwa marehemu na wenzake walikuwa katika sherehe ya Siku ya wapendanao duniani,ambapo marehemu aliuawa mita kadhaa kadhaa kutoka eneo la Grocery,huku ndugu wakisema marehemu aliuawa kwa sime na risasi kama inavyodaiwa na Jeshi la Polisi.

Kesi hiyo ambayo wananchi wengi walikuwa wakifuatilia inahusisha Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa kutumia Askari wake ambao ndio wanaodaiwa kusababisha kifo hicho.

Asasi mbalimbali zimekuwa zikilalamikia Polisi kujichukulia sheria mmkononi na kufanya vitendo vya unyanyasaji kwa wananchi wasiokuwa na hatia badala ya kufuata majukumu yao ya kazi kwa kushirikiana na jamii.

Kwa upande wake Mzazi wa marehemu,Bwana Godluck Mwakyusa amesema mwanae alimtegemea sana na tukio hilo limemfanya mara kadhaa kukosa amani,kufuatia majeraha ambayo mwanae alisababishiwa na Askari waliokuwa doria siku hiyo.
habari toka fullshangwe

No comments:

Post a Comment