KAMPENI ZA UCHAGUZI WA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI UDOM WAKOSA MVUTO,WANAFUNZI HAWATAKI SIASA
Mmoja wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha
Dodoma (UDOM) akinadi Sera zake kwa wanafunzi wenzake na kuomba kura
kwaajili ya wanafunzi kuweza kumchagua ili awe mbunge kutoka katika
Kitivo Cha sayansi ya Jamii.
Mwanafunzi mwingine naye aliweza
kuomba kura kwa baadhi ya wanafunzi ambao walihudhuria kampeni zake
katika kampeni zinazoendelea tayari kwa uchaguzi wa serikali ya
wanafunzi unaotarajiwa kufanyika june 2012
Hiyo Ndio kambi moja wapo katika
kampeni za kuwania nafasi mbalimbali katika serikali ya wanafunzi wa
UDOM wakiwa katika kampeni huku wengine wakisubiri kupiga kampeni kitu
ambacho wanafunzi wengi wamepuuzia na kudharau kampeni.
Wanafunzi Wachache waliojitokeza
kusikiliza kampeni za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika
serikali ya wanafunzi UDOM
Meneja Kampeni akiwapigia Debe
wagombea wake huku wanafunzi wengi wakiwa hawana habari na kampeni na
kuendelea na mambo yao kama wanavyoonekana pichani
Kuonyesha kwamba Siasa pamoja na
Kampeni zimekosa mvuto wakati wagombea wakinadi sera zao hao huku wao
wakitaniana kuhusiana na uchaguzi wa serikali ya wanafunzi hutakavyokuwa
na mwamko mdogo huku wengine wakisema hawatapiga kura kabisa kabisa
Hili ndio kundi la watu waliohudhuria kampeni za wagombea wa nafasi mbalimbali katika serikali ya wanafunzi UDOM.
No comments:
Post a Comment