Friday, June 8, 2012

KITABU CHA 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE MORNING) KIMEZINDULIWA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Bw. Walter Bugoya akitoa neno wakati wa uzinduzi wa kitabu cha 'FURAHA HUJA ASUBUHI' (JOY COMES IN THE MORNING) kilichoandikwa na Hopolang Phororo kinachozungumzia Mateso na manyanyaso ya wasichana wadogo wakati wa malezi yao na haki ya msingi ya jinsia ya kike katika jamii.
 Mmoja wa washiriki wa uzinduzi huo Bi. Chansa Kapaya akitoa neno la shukrani wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Hopolang Phororo na haki za msingi za wanawake wanaokutwa na matatizo ya unyanyasaji wa Kijinsia Tanzania.
Mtunzi wa Kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' Bi. Hopolang Phororo akielezea simulizi ya kweli iliyomkuta kama mwathirika wa unyanyasaji wa Kijinsia wakati wa usichana wake na moyo, uvumilivu aliokuwa nao wa kuweka uzoefu huo katika maadishi ili jamii ijifunze na madhara ya unyanyasaji wa Kijinsia unaokua kwa kasi nchini Tanzania.
Mgeni rasmi Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Fatma Mrisho akitoa nasaha zake wakati uzinduzi rasmi wa kitabu hicho jijini Dar es Salaam. Alisema 66% ya wanawake na 20% ya wanaume nchini wameshawahi kukutwa na majanga ya unyanyasaji wa Kijinsia  katika maelzi yao ambapo kwa sasa Dar es Salaam na Mbeya zinaongoza
 Mgeni rasmi Dkt. Mrisho na Mtunzi wakionyesha Kitabu kwa wageni waalikwa na waandishi wa habari. Kitabu hiki kinapatikana katika Maduka ya MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS  yaliyopo jijini Dar es Salaam kwa gharama ya shilingi 10,000/=.
Jopo la Wataalam wa Mambo ya Jinsia Tiba na Vitabu wakiwa kwenye picha pamoja.
 Mkurugenzi wa MKUKI NA NYOTA PUBLISHERS Mzee Bugoya akibadilishana mawazo na Dkt. Mrisho pamoja na Bi. Kapaya wakati wa uzinduzi
 Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa kitabu cha 'JOY COMES IN THE MORNING' uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wageni waalikwa wakibadilishana mawazo baada ya uzinduzi.

No comments:

Post a Comment