Tuesday, June 12, 2012

SHEAR ILLUSIONS, MUSTAFA HASSANALI WAJITOSA KUWADHAMINI MISS DAR INTER COLLEGE 2012


Baadhi ya warembo wanaotarajia kushiriki shindano la Miss Dar Inter College 2012, wakimsikiliza mwalimu wao, Marlydia Boniface, wakati wa mazoezi yao yaliyofanyika jana jioni kwenye hoteli ya Grand Villa, jijini Dar es Salaam.

***********************************
Na Mwandishi Wetu
WAKATI shindano la kumsaka  Miss Dar Intercollege 2012 likitarajia kufanyika Juni 22 kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa , uliopo mkabala na chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), duka la vipodozi la Shear Illusions, pamoja na mbunifu maarufu wa mavazi, Mustafa Hassanali, wamejitosa kudhamini shindano hilo.

Awali shindano hilo lilipangwa kufanyika juni 8 kabla ya kusogezwa mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo baadhi ya warembo kuwa katika mitihani pamoja na mafunzo yao kwa vitendo ‘Field’.

Akizungumza na mtandao  wa Sufiani Mafoto Blog, Mratibu wa Shindano hilo Dina Ismail, amesema kuwa, duka hilo la Shear,  lenye matawi yake jengo la Millennium Tower na Mlimani City linajihusha na uuzaji wa vipodozi halisi ‘original’ kutoka nje ya nchi litatoa vipodozi kwa warembo watakaoshiriki, huku Hassanali akiahidi kutoa zawadi ya magauni ya warembo.

Alisema maandalizi kwa ajili ya shindano hilo yanaendelea vizuri na leo warembo hao ambao awali walikuwa wakifanya mazoezi kwenye hoteli ya Lamada, watahamishia kambi yao kwenye hoteli ya Grand Villa iliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Dina ameongeza kuwa, mpaka sasa wameshapatikana warembo 13 ambao wapo chini ya ukufunzi wa Marylidya Boniface, huku kwa upande wa shoo wakinolewa na dansa mahiri katika miondoko ya Breack Dancer, Bob Rich.
“Mwaka huu tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,”alisema Dina.

Warembo watakaoshiriki shindano hilo  wanatoka vyuo vya  Biashara (CBE), Uandishi wa Habari (DSJ)  Time,  Ustawi wa Jamii,  Usimamizi wa Fedha (IFM)  na Chuo Kikuu huria (OUT, ambapo taji la mwaka 2011, linashikiliwa na Rose Msuya, kutoka IFM, huku mshindi wa pili akiwa ni, Blessing Ngowi, aliyetinga fainali za Miss Tanzania.

Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda  Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael, Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan.

Shindano hilo limedhaminiwa na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd’s,Dodoma Wine, Ndege Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa, Mustafa Hassanali, Grand Villa Hotel, Clouds Fm na blog za Michuzi, Mamapipiro, Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa Sufianimafoto na Fullshangwe.

No comments:

Post a Comment