Monday, June 11, 2012

MAXIMO KUTUA NCHINI KESHO TAYARI KWA KIBARUA CHAKE NA YANGA


  





















Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbrazil Marcio Maximo anatarajiwa kuwasili nchini kesho tayari kuanza kukinoa kikosi cha Yanga wana wa jangwani.
Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu amesema leo kwamba mara baada ya kuwasili Maximo atafanya taratibu za usajili kabla ya alhamisi kuanza rasmi kukinoa kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya michuano ya kombe la Kagame itakayoanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es salaam.







No comments:

Post a Comment