Sunday, April 29, 2012

Kwanini wanaume mnapenda kuterekeza Familia zenu?

LEILA SAIDI

Mimi ni mama wa miaka 40 sasa nina watoto 2 lakini nimetengana na mume wangu kwa miaka mitano sasa. Uniwie radhi kwa hii habari ni ndefu sana ila nataka kushare na wamama na wababa kwa ajili ya kile kinachotokea ktk maisha ya ndoa unapobainika udanganyifu kwa mmoja wapo.

Tumekuwa kwenye ndoa kwa miaka 11 mpaka nilipoamua kumuacha mume wangu January 2006, kwa muda wote tulioishi pamoja tulipitia maisha magumu na ya wastani na tulikuwa tunasaidiana sana. Nilikuwa nampenda mume wangu kwa dhati, akiwa hana kitu nilifanya kwa niaba yake na sikuona tatizo.

Mwaka 2002 mume alipunguzwa kazini na kwa maelezo yake hakulipwa hela ya maana, mimi nikaona sio tatizo nilikuwa na kipato cha kutuwezesha kuyamudu maisha ya familia yetu kwa furaha, hapo tayari nilikuwa nimenunua kiwanja maeneo ya Tegeta.

Mume alikuwa hayapendi maeneo hayo ya Tegeta hivyo hakujishughulisha hata kukiona hicho kiwanja. Muda mwingi mume wangu alikuwa anabaki nyumbani mimi nikiwa kazini. Hapo nyumbani tulikuwa na msaidiza wa kazi na watoto 2.

Wakati huo mtoto wetu mkubwa alikuwa anasoma darasa la 2 na mdogo alikuwa chekechea, nilikuwa na akiba niliokuwa naitunza kwa ajili ya kujenga lakini tukajadiliana tukaona bora tununue gari ili mume wangu awe na shughuli kwa kutumia hivyo gari. Mume wangu alitafuta gari nikalinunua na yeye akawa analitumua kama tax. Tatizo likaanzia hapo.

Naomba niwaambie hivi mimi ni mama mwaminifu ninamwamini Mungu katika kweli yote sikuwahi kumfikiria mume wangu vibaya au kama angaliweza kuwa na mwanamke mwingine au kutembea na house girl nilikuwa namwamini sana na nilikuwa bize sana nikidhani namsaidia mwenzangu kumbe wapi.

Gari lilianza kunionyesha mambo, mume akawa hataki kufanyia kazi akawa anazunguka nalo tu, asubuhi naulizwa hela ya mafuta, matengenezo mpaka nikajuta kununua hilo gari. Nikaamua kuwaambia ndugu zake waongee nae.

Walipoongea nae yeye akasema hawezi kuendesha taxi kama nataka ninunue fuso ndio atafanya kazi hiyo, hilo likaniwia gumu nikachukua gari nikampa dereva mwingine. Jamani! wakati mimi ninahangaika kutafuta pesa za matumizi na kusomesha watoto kumbe mwenzangu kaanzisha uhusiano na dada wa nyumbani ndio maana hata kazi hataki kufanya ila mimi nilikuwa sijui kinachoendelea.

Mwaka 2003 tulianza kujenga na yeye ndio alikuwa anasimamia ujenzi ila cha moto nilikiona, tunapanga bajeti ya site vizuri namkabidhi pesa akirudi jioni ana shoti laki 2 au laki inategemea na wingi wa pesa utakayompatia lazima apunguze materials bila sababu mpaka nikaanza kumchunguza.

Hapo tulikuwa tunaishi Kinondoni kumbe bila mimi kujua alikuwa kampangishia mwanamke chumba huko Gongo la Mboto. Tukaanza kukorofishana maana ukiweka hela ndani yeye kazichukua hata simu anabeba.

Alivyojua kuwa najua habari za huyo mwanamke akaanza kusema mimi nataka kumwacha kwasababu hana kazi, oh sababu unajenga na mambo mengi mabaya kwa kweli. Tulisuluhishwa lakini hakuwa tayari kuacha tabia ya wanawake wa nje na mimi nilimchukia sana kwa tabia zake ndicho kilichotutenganisha mimi na huyo mume wangu.

Tulipoamua kutengana aliniambia niondoke na watoto niliondoka nao na wanasoma vizuri tu kwani niliamua kuwapeleka Boarding School ili wasiadhirike na kutengana kwetu japokuwa wakirudi likizo Mume wangu anakuja kuwaona lakini hawasaidii kwa chochote hata chupi hawanunulii.

Kwa sasa anafanya kazi nzuri tu lakini hataki kuwasaidia watoto. Mwaka huu kabla watoto hawajarudi Shuleni waliniomba sana nimsamehe baba yao na nilifikiri sana nikawaita wazee na nikawaambia kuwa nimemsamehe kilichotushangaza ni kwamba yeye hajakubali kusamehewa anachotaka ni nyumba niandikwe kwa jina lake kwanza na gari ninalotumia nimpe au niliuze ndio atarudi.

Kwa masharti hayo mie nimesema basi na kila mtu aishi peke yake maana naona mwenzangu anawivu na nilichonacho ambacho kimsingi ni cha familia yetu, nimeogopa masharti yake maana anaweza kutufanya tuanze kupanga tena.

Kinamama ninachotaka kujua ni hiki; Kwa kina mama hivi waume zenu nao wakijua kuwa umejua anachokukosea na kutengana huwa wanawasusia familia?

..... na kina baba naomba kuwauliza mpaka lini mtawatesa wake zenu kwa kuwasusia familia zenu?

written by Leila Saidi

 


 • Murashani Gilbert PITA KWENYE TIMELINE YANGU JARIBU KUSOMA POST ZANGU KWA UMAKINI NA WEBSITE AU YOUTUBE NINAZOATTACH..NIMEADDRES SANA HILI TATIZO

 • Eric Goodluck kinachofanya watu kuishi mbali na familia zao mara nyingi ni utafutaji wa maisha. na inapotokea kuisahau familia basi itakuwa ni ulimbukeni tu! hakuna lingine.


 • Rojazz de Pain Dah pole sana

 • Francis Kitime for ya all watch out a Tyler Perry's "why did I get married" then be smart, for you maam, Im so sory for you bt be strong!


 • Waziri Zin Thi Kogvine P0le zake huyo dada maana......inategemea na akili ya mtu tu hlo jambo si kwa wanaume 2 bali hata kwa wanawake pia hutokea kuwafanyia waume zao mambo kama hayo...cha msingi ni kuaangalia mbele na kuhakksha unatunza vipi familia yako.

 • Rojazz de Pain Unajua cyo wanaume wote wenye tabia hzo inaelekea huyo mumeo hana mshipa wa aibu na haya na hajui misingi ya dini

 • Ally Mganzah pole sana dada kwa tatizo hilo lakini usiwalaumu wanaume tu bali hata wanawake wapo wanaoterekeza family siku hizi mapenz ya kweli hakuna ndio maana matatizo yote haya yanatokea mfano mimi pia niachwa na mke alipoenda kusoma Udom ndipo tatizo likaanza


 • Namwasi Mgonja so sorry sis,hawa wanaume huwa na hulka ya kutoridhika,na kibaya zaidi husahau walikotoka pindi tu wanapofanikiwa kimaisha.ki ukweli wanahitaji maombi.

 • Sent Denis Jerome Lekule pole sana,mama but sio wanaume wote,huyo alikuwa kabila gan?

 • Godwindaniel Reuben Urioh Stori ya kusikitisha kweli, pole sana dada na hongera kwa juhudi zako, achana naye atakupotezea muda wako tu huyo.


 • Alfa Chapalama
  Mimi ni mwanafunzi wa sheria SAUT, tumefundishwa kabla ya kutoa hukumu ni lazima uzipe pande mbili nafasi ya kusikilizwa, sasa hapa tumesikia upande mmoja tu wa mke lkn hatujamsikiliza mume, inawezekana kuna problem zilizomfanya afanye hivy...See More • Alfa Chapalama
  dada angu nakuomba kama mumeo hajaoa mke mwingine basi jitihada kusuluhisha ndoa yako irudi, mimi ni mtetezi wa haki za watoto kwa sababu nimeishi maisha ya kuungaunga kwa sababu ya msimamo wa mama angu kama wako, sipendi kuona watoto wanle...See More • Raphael Kalongola Ndoa inahitaji kuvumiliana,kuthaminia,na kujaliana,kuepuka kunyanyasana na kujishusha.Nina miaka 16 kwenye ndoa najionja namna ambavyo dada unapitia katika moyo wako na namna mwanamme anavyojihisi. Cha msingi kaa chini mzungumze myamalize,Hapa duniani hakuna aliye mkamilifu.Maoni yangu yangekuwa mengi kama yule bwana naye angetoa maelezo yake tukapima na kuyachuja.DADA SAMEHEANE MSIWAATHIRI WATOTO HAO KISAIKOLOJIA.


 • Charles Masaga
  Leila pole sana,


  Si kweli kwamba wanaume wote wako hivyo ila hilo ni tatizo na kwakuwa
  ni tatizo hilo dawa yake ndogo.


  ...See More • Sule Al-hinai
  LEILA mimi nikiwa kama muislam thabit na mwenye imani na dini yetu pls usije ukaingia kanisani kwa ajili ya maombi kama alivyosema bwana masanja kwani dini yetu inasema WAIDHA SAALAKA IBADI ANNY FAINNI KARIBU UUJIB DAWAATI DAI WAIDHA DAANI ...See More • Joshua Nkuku
  Leila pole kwa matatizo ya kutelekezwa na mme. Ninavyojua binadamu sio rahisi kuwa na tabia moja. Km mtetezi wa watoto ni vema watoto wakapata haki ya kulelewa na wazazi wote wawili. Mimi siamini km kweli wanaume wote wanaweza kuwa na tabia...See More • Joshua Nkuku
  Leila pole kwa matatizo ya kutelekezwa na mme. Ninavyojua binadamu sio rahisi kuwa na tabia moja. Km mtetezi wa watoto ni vema watoto wakapata haki ya kulelewa na wazazi wote wawili. Mimi siamini km kweli wanaume wote wanaweza kuwa na tabia...See More


 • Joshua Nkuku
  Leila pole kwa matatizo ya kutelekezwa na mme. Ninavyojua binadamu sio rahisi kuwa na tabia moja. Km mtetezi wa watoto ni vema watoto wakapata haki ya kulelewa na wazazi wote wawili. Mimi siamini km kweli wanaume wote wanaweza kuwa na tabia...See More

 • Alfa Chapalama
  kama alivyosema joshua, naomba fanya kitu kimoja hiyo nyumba andikisha majina yenu wote au unaweza kuandika jina la mwanao mkubwa, then hilo gari unaweza kuuza afu fedha kaweke kwenye akaunt yako. then mwambie huyo mumeo atafute mahari pa k...See More


1 comment: