Monday, April 30, 2012

Airtel Yatoa Msaada Wa Computer na Vitabu Kwa Chuo Kikuu Cha Dodoma

Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando akikabidhi baadhi ya vitabu  vya chuo kikuu vilizotolewa na Airtel kwa chuo kukuu cha Dodoma (UDOM) kwa Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idrisa Kikula (kulia) jana wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika chuoni hapo.  anaeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa (kati). Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS ikiwa ni muendelezo wa Airtel katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.
Mkuu wa wilaya ya Bhahi Bi Betty Mkwasa, akiwa na Makamu Mkuu wa chuo cha Dodoma (UDOM) jana pamoja na wafanyakazi wa Airtel na baadhi ya wanafunzi wa IT chuoni hapo wakiwa wameshikilia vitabu vilivyotolewa msaada na Airtel kwa chuo hicho wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vitabu 104 na kompyuta 20 vyote vyenye  thamani ya milioni 25/- TZS  toka Airtel ikiwa ni muendelezo wa Airtel kuchangia sekta ya Elimu nchini.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu 104 na computer 20 vyote vyenye thamani ya milioni 25/- TZS kwa chuo kikuu cha Dodoma ikiwa ni muendelezo wa shughuli zake za kijamii  katika kuchangia sekta ya Elimu nchini.

Komputa hizo pamoja na vitabu  vimekabidhiwa  kwa Makamu Mkuu wa chuo cha UDOM kilichopo mkoani Dodoma jana wakati wa hafla fupi iliyofanyika ukumbi mdogo wa mikutano chuoni hapo na kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Bhahi Mh, Betty Mkwasa

Akiongea wakati wa makabidhiano hayo Mkuu wa wilaya wa Bhahi aliishukuru Airtel Tanzania kutokana na jitihada zake za kushirikiana na serikali katika kusaidia sekta mbali mbalimbali ikiwemo elimu

 “Hili ni tukio muhimu sana mnalofanya Airtel na  inaonesha dhahiri dhamira yenu ya kushirikiana na serikali yetu na jamii kwa ujumla kuchangia elimu ili kuinua kiwango cha elimu nchini, hivyo kufanya hivi nchi yetu inafaidika sana”

“ninawaomba wanafunzi kuhakikisha mnavitumia kikamilifu kompyuta na vitabu hivi ili kujiongezea ujuzi na uelewa zaidi katika masomo kwa manufaa yenu na  kwa taifa pia” alimaliza kusema Mh Mkwasa

Nae  Meneja uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando alisema”  Airtel chini ya mpango wetu maaalum wa kuchangia elimu bado tutaendelea kuchangia  elimu nchini, leo tunaona fahari sana kuweza kujitolea sehemu ya faida yetu pia kwa taasisi ya elimu ya juu (UDOM),  msaada wetu huu wa kompyta 20 na vitabu 104 vya elimu ya juu ni muendelezo wa mpango wetu wa *Airtel Shule Yetu *uliodumu kwa zaidi ya miaka saba ukiwa ni maalum kwa kuchangia elimu

 “kwa kupitia mpango wa Airtel Shule yetu  tumeshanikiwa kuzifikia zaidi ya shule 800 na kutoa msaada wa vitabu na vifaa vya kufundishia yakiwemo pia madawati”

Kwa mwaka 2012-2013  bado Airtel tunaendelea na dhamira yetu ya kusaidia sekta ya elimu katika nyanja tofauti ikiwapo; kutoa madawati kwa shule za msingi na sekondari, kurekebisha majengo ya shule, kutoa computer kwa shule za sekondari na vyuo lengo hasa likiwa ni kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu bora ili kuweza kupata nguvu kazi ya kesho na kulikomboa taifa katika swala la umaskini na elimu duni.

Nae Makamu Mkuu wa Chuo cha Dodoma (UDOM)  Profesa Idrisa Kikula aliishukuru Airtel na kuongeza kuwa msaada huo wa kompyuta na vitabu umeenda wakati muafaka na unahitajika sana.

“Vitabu na komputa hizi ni muhimu kwa chuo kikuu chetu cha Dodoma, tunaamini kabisa vitabu hivi  vitasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uhaba wa vitabu na zaidi kuwapatia wanafunzi na walimu nyenzo za kujisomea na kufundishia pia” alisema Profesa Idrisa Kikula Makamu mkuu wa chuo UDOM

 “Msaada huu umekuja muda muafaka kwa kuwa Komputa ni muhimu sana kwa elimu ya juu ukizingatia karne hii ya sayansi na teknololojia  hivyo zitatumika kufundishia masomo mbalimbali ya ICT na kuwapa wanafunzi ujuzi wa teknolojia ya habari na sayansi ya kompyuta” alimaliza kwa kusema Profesa Idrisa Kikula Makamu mkuu wa chuo UDOM

Chuo kikuu cha Dodoma ambacho ni maarufu kama UDOM kilifunguliwa rasmi mwaka 2007 huku kikiwa  na sifa ya kuwa na maabara kubwa (library) kuliko chuo chochote cha elimu ya juu kilichopo nchini. Kwa sasa chuo hicho kinakadiriwa kuhudumia zaidi ya wafunzi 20,000 nchini huku matarajio ni kufikisha wanafunzi kutoa elimu kwa wanafunzi 40,000 kwa siku zijazo.

No comments:

Post a Comment