Sunday, June 3, 2012

MAMIA YA WATANZANIA WAJITOKEZA KWENYE MBIO ZA SUSAN G.KOMEN 2012 KUMALIZA VITA DHIDI YA MARADHI YA SARATANI YA MATITI.


Wananchi wakiwemo Watanzania walikusanyika katika viwanja vya Down Town Washington DC siku ya Jumamosi June,2,2012 katika kuitikia wito wa kuunga mkono wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa saratani ya maziwa, utafiti na elimu dhidi ya ugonjwa huo.
Tukio hili lilianza kwa matembezi ya vikundi vya mataifa mbali mbali wanaoishi nchini Marekani.
Watembeaji wengi waliohudhuria katika matembizi hayo kutoka majimbo mbali mbali nchini Marekani. Maradhi ya saratani ya maziwa yanakisiwa kuwadhuru watu 25 milioni kote ulimwenguni ambapo kama hatua haitochukuliwa inakisiwa watu milioni 10 kufa katika kipindi cha miaka 25 ijayo.
Kina dada wakiwa katika matembezi ya kupiga vita ogonjwa wa saratani ya maziwa siku ya Jumamosi June, 2, 2012 ndani ya Washington D.C nchini Marekani.
Rais wa Jumuia ya waTanzania DMV Mh. Iddi Sandaly, wa kwanza kushoto, Waheeda Margaret Gathesha, Chief wa swahilivilla Abou Shatry, Aunt Rehema, pamoja na Salma Jay Jay pia alikuwepo katika matembezi ya kupigana na ugonjwa wa saratani ya maziwa Washington DC.
Wazawa wa Kitanzania wanaoishi nchini marekani wakiwa katika matembezi ya kupiga vita ugonjwa wa saratani ya maziwa mapema ndani ya Washington D.C nchini Marekani.
Warembo wa kiTanzania wakiwa mstari wa mbele katika mpango mzima wa kutimiza mwendo wa mile tatu.
Team Tanzania wakipata picha ya pamoja  katika kuitikia wito wa kuunga mkono wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa saratani ya maziwa, utafiti na elimu dhidi ya ugonjwa huo.
Mamia ya watu kutoka sehemu mbali mbali waliungana kwa pamoja  katika zowezi hilo la kuunga mkono wanawake ambao wanakabiliwa na ugonjwa wa Saratani ya maziwa.
Wananchi wakiwa katika mwendo wa Susan G.Komen. kumaliza vita dhidi ya maradhi ya Saratani ya Maziwa Susan G.Komen. 2012!
Kina kaka nao pia hawajajiweka nyuma kuunga mkono Susan G.Komen. kumaliza vita dhidi ya maradhi ya Saratani ya Maziwa Susan G.Komen. 2012! ndani ya Washington DC.
Ahsanteni sana Auntie Rehema na Dada Zuhura, kwa kutupa muamko wa kuwajibila na kushiriki katia zowezi haya hili la kupiga vita ugonjoa huu wa satarani ya maziwa. M/mungu akujalie Afya njeema Insha-Allah Ameen.!
Team Tanzania baada ya kumaliza matembezi ya Susan G.Komen. dhidi ya kupiga vita  maradhi ya Saratani ya maziwa.

No comments:

Post a Comment