Saturday, June 30, 2012

WANAHARAKATI WALIPOKUWA WANAMUAGA DR, ULIMBOKA KWENDA NG'AMBO KWA MATIBABU ZAIDI

 Wanaharakati leo walipomuaga Dkt. Ulimboka kwenda n'gambo Ni katika Uwanja wa Ndege wa Kimtaifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam wakati wa  kumsindikiza Dkt. Ulimboka  kwenda ng'ambo kwa ajili ya  vipimo vya ziada na matibabu  stahiki baada ya majibu ya vipimo  hivyo ambavyo imeshindikana kuvipata nchini kutokana na ama kuharibika kwa vifaa hivyo au kukosekana kabisa.
Mabango ya Madaktari,
 Umma hauna budi kutambua kuwa bila ya vipimo sahihi, ni  vigumu sana kutoa matibabu sahihi. Wagonjwa wengi  wamepoteza uhai kutokana na kukosekana vipimo kwa ajili ya  kufanya uchunguzi mbalimbali
 kabla ya kufikia uamuzi  "diagnosis" kwa ajili ya matibabu  sahihi, na hivyo Madakari  wamebaki wakitumia zaidi uzoefu wao.
 Hili ni mojawapo ya mambo  ambayo Madaktari wamekuwa  wakijitahidi kulieleza na kutaka  lifanyiwe kazi na Serikali, ili  waweze kutumia vyema kisomo  chao na kukuza uwezo wao wa  kutafiti na kutibu magonjwa  mbalimbali. Kukosekana kwa vifaa ndiyo moja ya mambo makubwa
 kabisa yanayochangia wagonjwa  wanapelekwa nje ya nchi. Ukweli wa usemi huu unadhihirika pale Madaktari wa  Kitanzania wanapohamia nchi za  ng'ambo na kufanya kazi katika  nchi hizo kwa ufanisi. Ikiwa Madaktari hawa wasingekuwa na  uwezo na maarifa, haiyumkini  wasingeweza kufanya kazi huko waendako.
 Dkt. Ulimboka ameondoka akiwa  chini ya ulinzi mkali wa Madaktari  huku wanaharakati, baadhi ya  madaktari na wananchi  wakereketwa wakionesha  mabango ya kulaani unyama aliofanyiwa Dkt. Ulimboka
 Source:wavuti.com

SHEREHE ZA MAHAFALI YA WAHITIMU WA SHAHADA YA KWANZA LUMUMBA UNIVERSITY, RUSIA

 Katika chuo kikuu cha ushirikiano wa kimataifa kilichopo nchini Rusia, LUMUMBA PEOPLE FRIENDSHIP UNIVERSITY, Rusia Wanafunzi wakitanzania wasomao nchini Russia waungana na wenzao wanaotoka nchi mbalimbali duniani katika mahafali ya wahitimu wa shahada ya kwanza waliokuwa wakisoma chuo kikuu cha Lumumba nchini Russia,

Katika mahafali hayo yalio jumuisha wanafunzi wakitanzania waliohitimu shahada tofauti tofauti zikiwemo shahada ya computer, technologia ya usafirishaji na udaktari, Wadau hawa wakiwa wenye furahaa walisema
"Tunamshukuru mungu kwa kumaliza safari hii, na tunaishukuru sana Rusia kwa kutulea na kutupa msaada kufanikisha malengo yetu yakupata elimu na ujuzi tulio hitaji, na tunaahidi kurejea nyumbani na kutumia ujuzi na elimu hii tulioipata huku kwa manufaa ya taifa letu na watanzania wote,
Tungependa kuwasisitiza wanafunzi wote waliopo nchini Tanzania wajitahidi kujakusoma nje ya nchi kwani kuna nafasi nyingi za kusoma utakacho na kufanya vizuri, Maisha ya ughaibuni yana wezekana "
Habari picha, Na repoter wetu kutoka Urusi,,,!!
Wanafunzi wakiafrica waliohitimu shahada ya kwanza katika chou kikuu Lumumba, Rusia

Ukimaliza chuo unasikia raha yaaa jabuu,,,, hapa niwalio hitimu wakionyesha furaha zao

vijana walio hitimu wakichuo picha ya pamoja na wanafunzi wengine

wadau in da poz,,,,,



Mdau aliyehitimu shahada ya kwanza

Thursday, June 28, 2012

Matukio mbali mbali hospitali ya Muhimbili leo baada ya Dkt Ulimboka Kufikishwa Muhimbili akiwa mahututi

Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpakia kwenye Gari Daktari Mwenzao aliepatwa na Mkasa wa Kutekwa Nyara na watu wasiojulikana na ambao walimjeruhi vibaya sana,Dk. Steven Ulimboka aliepatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo huko katika msitu wa Mabwepande,jijini Dar
Wanahabari wakihangaika kupata picha ya Dk. Steven Ulimboka alieinginzwa kwenye gari hiyo tayari kwa kupelekwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakilisukuma gari lililokuwa limempakia Dk. Steven Ulimboka.
Madaktari na Wauguzi wa Muhimbili wakiwa wamesimama huku wakizungumzia hali iliyompata mwenzao.
Mwanahabari akiwa katika harakat za kupata picha makin na mahiri
Hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati Dk. Ulimboka alipofikishwa hospitalini hapo.Picha Zote Kwa Hisani ya Michuzi Blog

UP-DATE: Dkt Ulimboka azungumza kilicho mpata

Mweneyikiti wa Jumuia ya Madaktari nchini Dk Stephen Ulimboka, amepigwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika.
Dkt Ulimboka anadaiwa kuvunjwa mbavu, miguu yote miwili, kung’olewa meno yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio hilo la kikatili na kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia leo jijini Dar es Salaam, na linadaiwa kufanywa na watu wa sio julikana ambapo kabla ya kufanya unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kabla ya kumtelekeza katika eneo la msitu wa Pande Mabwepande.
DKT. ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO
Akisumulia tukio hilo Dkt Ulimboka alisema kuwa  jana usiku alipigiwa simu na mtu aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji kuongea naye, na ndipo walipopanga kuonana katika eneo la Leaders Kinondoni.
Dk Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla, alikuwa na wasiwasi kwani kila mara alikuwa akipokea simu na kuwasiliana na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.
Alisema baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye rangi nyeusi na kuondoka naye.
Dkt Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga, na kumfikisha katika msitu huo wa pande na kuendelea kumpiga paka alipoteza fahamu.
MADAKTARI NAO WALONGA
Akisimulia mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt Deo, alisema kuwa alipigiwa simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha tukio hilo.
Alisema alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo la usoni.
Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.
"Hali yake kwakweli ni mbaya sana, amepigwa mno na ameumizwa kwakweli tumemleta hapa hili aweze kupata matibabu, lakini mimi nilivyomkuta mara ya kwanza nilishindwa hata kumtambua kwa jinsi alivyokuwa ameumizwa"alisema Dkt Deo
Alisema kuwa alisimuliwa na Dkt Ulimboka kwamba watu hao waliomteka na kumpiga walikuwa na silaha na kwamba alishindwa kuwatambua.
Aliongeza kuwa Dkt Ulimboka alidai kuwa wakati akiwa katika halimbaya alikuwa akisikia mazungumzo yao, wakibishana juu ya kumuua wengine wakisisitiza achomwe sindano, na wengine wakitaka kumpiga risasi.
Alisema wakati mabishano yakiendelea kati yao, Dkt Ulimboka aliinuka akiwa na lengo la kukimbia lakini watu hao walipiga risasi hewani iliyomshtua na kuangua chini.
Kwa upande wake Dkt Cathbeth Mcharo ambaye ndiye aliyempokea Dkt Ulimboka Hospitalini hapo, alisema kuwa hali yake ni mbaya na kwamba wanajitahidi kumpatia huduma za haraka.
Alisema kuwa kwa hatua za awali amefanyiwa vipimo mbalimbali, hili iweze kufahamika aina ya matibabu anayotakiwa kupatiwa.
POLISI
Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo
MUHIMBILI
Wakati hayo yakitokea inadaiwa kuwa Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo kikali kutoka kwa madaktari hapo Muhimbili kwa kile kilochodaiwa kutambuliwa na Dkt Ulimboka kuwa mmoja wa watu walio mjeruhi.
Pia inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia chooni na kufanya mawasiliano na wenzake huku Madaktari hao wakimsikiliza na kutokana na alichokua akiongea chooni humo ndipo alipotoka aliambulia kichapo kikali.
Pia baadhi ya madkatari na wauguzi walikuwa wakisukuma gari alilokuwa amepanda Dkt Ulimboka huku wakiimba nyimbo za Umoja na Mshikamano Daima miongoni mwao.
Hali ya ulinzi ilikuwa kali Hospitalini hapo kwani Picha zilikuwa haziruhusiwi kupigwa.Source Father Kidevu Blog

MWAKA WA 3 UDOM WANAPOANGAIKA NA ZOEZI LA CLEARANCE.WANAFUNZI WALALA KWENYE OFISI ZA WAHASIBU NA WENGINE KUFIKA SAA SABA USIKU

Baadhi ya wanafunzi wa Mwaka wa 3 wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ambao wanahitimu masomo mwezi baada ya kumaliza mitihani ya mwisho hatimaye wahangaika na zoezi la kufanya clearance katika ofisi za wahasibu.Baadhi ya wanafunzi wamelala katika ofisi za wahasibu na wengine kufunga safari saa saba usiku yote ni kwaajili ya kuwahi ili waweze kumaliza mapema zoezi hilo na hatimaye wawe huru kabisa.
Wahitimu hao wakiwa kwenye foleni tokea saa saba usiku.Huku wengine wakiwa wamelala mlangoni mwa ofisi ya wahasibu na huku wengine wakifika ofisini hapo saa saba usiku.Du kazi kweli

Wednesday, June 27, 2012

JIHADHARINI NA UTAPELI HUU

Kutokana na Kupenda Kuchunguza Mambo hususani ya msingi sana. Niliona Tangazo la Kazi Kupitia moja ya Blogu za Hapa tanzania nilihisi lakini Sikupenda Kuhukumu bila Kuwa na ushahidi na ufahamu wa kutosha kuhusu hilo Swala.

Hilo tangazo lilikua ni La Kazi nikaomba baada ya hapo wakaniambia nitumie CV, na kujibiwa kuwa baada ya Siku Mbili za Kazi nitajibiwa. Niliomba hiyo nafasi wiki iliyopita na Jana Nikajibiwa na Huu hapa Chini Ndio Ujumbe niliotumiwa na Hao Wahuni wa Mtandaoni ..

Habari,

Ninayofuraha kukufahamisha kuwa ombi lako la kufanya kazi na Mercycorps Nicaragua(Central America) limekubaliwa,nimeambatanisha barua ya kukubaliwa ambayo utasaini panapohusika na kuirudisha kwetu.
Kwa mujibu wa sheria za immigration hapa Nicaragua,NGO inatakiwa kukuombea Visa/work permit ili uweze kuja hapa kuanza kazi,kwa sasa hakuna ubalozi wa Nicaragua hapo Tanzania.
Kama ambavyo nilikutaarifu hapo awali unatakiwa kutuma malipo kwa ajili ya kuprocess Visa/Work permit yako mapema kama ambavyo barua ya kukubaliwa kazi inavyojieleza ili kutoa muda mzuri kwa NGO kuprocess kwa wakati ambapo itachukua siku 4 za kazi kupata kibali hicho cha Visa/Work permit.

Sasa katika kurahisisha utumaji wa malipo hayo Management imeomba kutumia account ya mfanyakazi ambaye yeye ana account ambayo ni International Account ambayo benki yake pia inapatikana hapo nchini Tanzania,hii ni kwa sababu ya kurahisisha na kuondoa gharama za utumaji na ucheleweshaji wa kupata malipo kwa wakati.
Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kubadili hiyo dola $197 kuwa Tanzania shillings ambayo ni sawa na  Tsh.315,200/- ,harafu utadeposit hiyo Tsh.315,200/- kwenye account ifuatayo;
Tafadhali nakuomba uscan na unitumie payslip/Deposit slip baada ya kufanya malipo kwa Sababu Management itaihitaji kwa sababu za kiofisi,


Bank Name: Stanbic Bank
Account Name: Jacob E.E
Account Number: 0140518946701
Visa Card Number: 4313321007132065

Regards
Lilian Kisanga
Project Manager
Mercycorps
Nicaragua
Kutokana na Ujumbe huo Niliingiwa na Wasiwasi Sana na kujiuliza vitu vifuatavyo: Iweje Swala la Kulipa pesa ya Visa/Work Permit niliambiwa ni USD 197 iweje sasa Nilipe kwa Tsh? Halafu pili Iweje Nilipe kwenye Account ya Mtu binafsi? Baada ya hapo Ikabidi nifuatilie kuhusu hii account ikanibidi niwasiliane na Stanbic Bank kwaajili ya Ufafanuzi zaidi na Ubalozi wa Marekani.Huu hapa Chini ni Ujumbe niliopokea Kutoka Benki ya Stanbic Bank.....unasomeka hivi 
"
Habari Josephat,
Unashauriwa kwamba kwa sasa usiweke hela yoyote kwenye hiyo akaunti ya Jacob E.E.
Salamu,
Patricia
"
Ndugu Zangu Huu Ni Utapeli Kwahiyo Msitume

ALGERIAN NATION EXAMINATION RESULTS,,, STUDENTS ARE SO FUNNY,,,!!

Result of the Algerian Nation Exams ,,,,!!!! Welcome  to University guys,,,,,,!!!!!
this is how they say,,,,,,
"a small thought has those who pass the tray and awaiting the results"
Photo: True
(Translated by Bing)
Photo: une petite pensée a ceux qui ont passer le bac et qui attendent les résultats
–

Sunday, June 24, 2012

Miss Dar InterColledge 2012 wazidi kujifua


Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Dar Inter Collodge 2012, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika Hoteli ya Grand Villa Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Shindano hilo litakalo pambwa na Burudani kutoka kwa Diamond linataraji kufanyika Ijumaa Juni 22, 2012 katika Ukumbi wa Makumbusho jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). 
Warembo wanaoshiriki shindano la Miss Dar Inter Collodge 2012, wakifanya mazoezi ya wimbo wao wa ufunguzi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika Hoteli ya Grand Villa Kijitonyama Jijini Dar es Salaam. Shindano hilo litakalo pambwa na Burudani kutoka kwa Diamond linataraji kufanyika Ijumaa Juni 22, 2012 katika Ukumbi wa Makumbusho jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).

TANZANIA NA CHINA WAJIVUNIA MAFANIKIO YA MATUMIZI YA TEKNOLOGIA

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza jambo na Balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing wakati wa hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya  China na Tanzania kwenye miradi mbalimbali ya kilimo nchini.
Viongozi mbalimbali kutoka ubalozi wa China na seraikali ya Tanzania wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania kabla ya kuanza  hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya  China  na Tanzania kwenye miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania.Kutoka kushoto nyuma ni balozi wa China nchini Tanzania Bw.Lu Youqing, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule.
Baadhi ya mashuhuda wa miradi mbalimbali ya ushirikiano kati ya China na Tanzania ukiwemo ujenzi wa  reli ya Uhuru (TAZARA) walioalikwa kwenye hafla hiyo  Bw. Abdul Haji (kulia) na mama Roza Kangoma (kulia) ambaye ni mama wa balozi wa Zambia nchini Tanzania pia aliwahi kuwa mkuu wa chuo cha mafunzo cha TAZARA.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Eng. Christopher Chiza (kulia) akizungumza na wageni mbalimbali walioalikwa na ubalozi wa China nchini Tanzania kuhusu  mikakati ya serikali ya kuboresha  kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao wakati wa hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kati ya China na Tanzania katika miradi mbalimbali ya Kilimo inayofanyika Tanzania.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo katika ubalozi wa China nchini Tanzania wakifuatilia masuala mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
Raia kutoka mataifa mbalimbali waliohudhuria hafla fupi ya kusherehekea   mafanikio ya matumizi ya teknolojia ya kilimo kutoka nchini China katika miradi mbalimbali inayofanyika nchini Tanzania wakijipatia nakala mbalimbali za machapisho kuhusu shughuli za kilimo, siasa, Utamaduni, Teknolojia na masuala ya kijamii.
Picha na Aron Msigwa -MAELEZO

KESI YA MWANAFUNZI WA TEKU ALIYEUAWA NA POLISI KUANZA KUSIKIKA MAHAKAMA KUU HIVI KARIBUNI - MBEYA


 Baadhi ya majeraha yaliyotokana na kipigo kwenye mwili wa marehemu Daniel  Godluck Mwakyusa (31) ambaye alikuwa mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU),Mbeya aliyeuawa na Askari wa Jeshi la Polisi mkoani hapa tarehe 14/02/2012 katika sikukuu  ya wapendanao {valentine day].
******
Habari na Mwansidhi wetu,Mbeya.
Kesi ya mwanafunzi anayedaiwa kuuawa na Polisi Mkoani Mbeya,itaanza kusikika Juni 27 mwaka huu katika Mahakama Kuu,jijini Mbeya.

Mwanachuo huyo anayedaiwa kuuawa na Polisi marehemu Daniel Mwakyusa,aliyekuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU) kilichopo jijini hapa,tukio lililotokea Februari 14 mwaka huu.

Imedaiwa marehemu na wenzake walikuwa katika sherehe ya Siku ya wapendanao duniani,ambapo marehemu aliuawa mita kadhaa kadhaa kutoka eneo la Grocery,huku ndugu wakisema marehemu aliuawa kwa sime na risasi kama inavyodaiwa na Jeshi la Polisi.

Kesi hiyo ambayo wananchi wengi walikuwa wakifuatilia inahusisha Jeshi la Polisi mkoani Mbeya kwa kutumia Askari wake ambao ndio wanaodaiwa kusababisha kifo hicho.

Asasi mbalimbali zimekuwa zikilalamikia Polisi kujichukulia sheria mmkononi na kufanya vitendo vya unyanyasaji kwa wananchi wasiokuwa na hatia badala ya kufuata majukumu yao ya kazi kwa kushirikiana na jamii.

Kwa upande wake Mzazi wa marehemu,Bwana Godluck Mwakyusa amesema mwanae alimtegemea sana na tukio hilo limemfanya mara kadhaa kukosa amani,kufuatia majeraha ambayo mwanae alisababishiwa na Askari waliokuwa doria siku hiyo.
habari toka fullshangwe

VYUO VIKUU 60 VYA AFRIKA MASHARIKI KUSHIRIKI MAAONYESHO JIJINI ARUSHA



Na.Ashura Mohamed-Arusha
Vyuo vikuu 60 zikiwemo taasisi za elimu ya juu na wadau wa vifaa mbalimbali vya elimu kutoka  nchi za Afrika mashariki  wanatarajia kushiriki katika maonyesho  ya huduma na bidhaa zao yatakayofanyika mwezi ujao mjini Arusha.

Mratibu wa maonyesho hayo Peter Oguwi amesema  maonyesho hayo yatakayoanza julai 10 hadi 14 yatafanyika katika viwanja vya nane nane njiro.

Pia  nyatashirikisha vyuo kutoka nje ya afrika mashariki ikiwemo India maonyesho ambayo ameyaelezea kuwa ni ya kipekee na mara ya kwanza kufanyika na yanatarajia kuleta watu zaidi ya 500.

Oguwi amesema lengo la maonyesho hayo ni kutangaza huduma zinazotolewa na vyuo hivyo zikiwemo program mbalimbali ilikuwafanya wananchi wanchi hizo kuthamini vyuo vyao badala ya kukimbilia nchi za nje hivyo maonyesho hayo yana  tarajia kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu ya juu.

Waziri wa elimu na ufundi Shukuru kawambwa anatarajiwa kufungua rasmi maonyesho hayo July 11 mwaka huu Jijini Arusha.

Chemi & Cotex kwa kushirikiana na Mgulani shule ya msingi watembelea kituo cha Yatima cha Friends of Don Bosco Kimara.

Piscus Laswai ambaye pia ni mmoja wa yatima wanaolelewa na kituo cha Friends of DonBosco kilichopo Kimara jijini akipokea zawadi ya taa zinazotumia mwanga wa jua kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Mgulani ambazo zitawasaidia yatima hao kujisomea hasa nyakati za usiku kunapokua na tatizo la umeme.
 
Mwanafunzi wa darasa la saba kutoka shule ya msingi Mgulani Emmanuel George (kulia) akiwapa zawadi ya mpira wanafunzi wenzake ambao ni yatima wanaolelewa katika kituo cha Friends of DonBosco kilichopo Kimara pindi walipotembelea kituo hicho hivi karibuni chini ya uwakilishi wa Chemi & Cotex ltd.
Watoto yatima wanaoishi kituo cha Friends of DonBosco kimara jijini wakiwakaribisha wanafunzi kutoka shule ya msingi Mgulani kituoni hapo pindi walipokuja kuwatembelea yatima hao na kufahamiana zaidi hasa kielimu pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali zenye thamani ya shilingi milioni moja kutoka kampuni ya Chemi & cotex.

Watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Friends of Don Bosco kilichopo Kimara jijini wakifurahia zawadi za miswaki na dawa za meno za Whitedent walizopewa na wanafunzi wenzao kutoka shule ya msingi Mgulani waliowatembelea kituoni hapo hivi karibuni ikiwa ni sehemu ya kufamiana zaidi katika maendeleo ya elimu kwa ujumla.

PRECISION AIR KUANZA SAFARI ZA DAR ES SALAAM HADI LUSAKA

Zambia waishukuru Precision Air kuanza Safari za Dar es Salaam hadi Lusaka

Mkurugenzi Mkuu na CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi wa safari za Shirika hilo la ndege jana kutoka Dar es Salaam hadi Lusaka Zambia kupitia Lubumbash.Hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz.

 Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Grace Mujuma akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
  Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Uchukuzi, John Thomas James Mngodo akizungumza kaatika hafla hiyo iliyofanyika katika mji wa Lusaka Hoteli ya Taji Pamodz.
Mgeni Rasmi, Naibu Wazizi wa Usafirishaji, Kazi, Usambazaji na mawasiliano wa Zambia, Samuel Mukupa akizungumza jana katika tafrija maalum ya uzinduzi wa safari za Ndege za Kampuni ya Precision Air kutoka Dar es Salaam kwenda Lusaka kupitia Lubumbashi. Mukupa alisema mbali ya kuzidisha mahusionao baina ya Tanzania na Zambia lakini pia itawasaidia sana wafanya biashara wa Zambia katika safari zao za kibiashara Tanzania.
Wageni mbalimbali wakifuatilia tafrija
Meneja Mkazi wa Afrika ya Kati wa Kampuni ya Precision Air, Emmanuel Mathias Ng'andu akiwa na Meneja Maweasiliano wa Kampuni hiyo Anneth Nkini wakati wa tafrija hiyo.
Viongozi wakishangilia jambo.
Wageni mbalimbali wakiwepo na wafanyakazi wa Precision Air wakifuatilia matukio.
CEO wa Precision Air, Alfonse Kioko (kulia) akiwaongoza wafanyakazi wake kucheza EDUDHA
Mkurugenzi wa Masoko, Patriki Ndekana , (kushoto), Meneja Mauzo, Tuntufye Mwambusi, Hilda Lema, Mariam Ismail na Meneja Mkazi wa Afrika ya Kati wa Kampuni ya Precision Air, Emmanuel Mathias Ng'andu wakipamba moto katika EDUDHA.
Kocha Msaidizi wa Mabingwa wa Afrika, Timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' Honor Janza nae alikuwepo. SOURCE:FATHER KIDEVU BLOG