Kwanini wanaume mnapenda kuterekeza Familia zenu?
|
LEILA SAIDI |
Mimi ni mama wa miaka 40 sasa nina watoto 2 lakini nimetengana na mume
wangu kwa miaka mitano sasa. Uniwie radhi kwa hii habari ni ndefu sana
ila nataka kushare na wamama na wababa kwa ajili ya kile kinachotokea
ktk maisha ya ndoa unapobainika udanganyifu kwa mmoja wapo.
Tumekuwa kwenye ndoa kwa miaka 11 mpaka nilipoamua kumuacha mume wangu
January 2006, kwa muda wote tulioishi pamoja tulipitia maisha magumu na
ya wastani na tulikuwa tunasaidiana sana. Nilikuwa nampenda mume wangu
kwa dhati, akiwa hana kitu nilifanya kwa niaba yake na sikuona tatizo.
Mwaka 2002 mume alipunguzwa kazini na kwa maelezo yake hakulipwa hela
ya maana, mimi nikaona sio tatizo nilikuwa na kipato cha kutuwezesha
kuyamudu maisha ya familia yetu kwa furaha, hapo tayari nilikuwa
nimenunua kiwanja maeneo ya Tegeta.
Mume alikuwa hayapendi
maeneo hayo ya Tegeta hivyo hakujishughulisha hata kukiona hicho
kiwanja. Muda mwingi mume wangu alikuwa anabaki nyumbani mimi nikiwa
kazini. Hapo nyumbani tulikuwa na msaidiza wa kazi na watoto 2.
Wakati huo mtoto wetu mkubwa alikuwa anasoma darasa la 2 na mdogo
alikuwa chekechea, nilikuwa na akiba niliokuwa naitunza kwa ajili ya
kujenga lakini tukajadiliana tukaona bora tununue gari ili mume wangu
awe na shughuli kwa kutumia hivyo gari. Mume wangu alitafuta gari
nikalinunua na yeye akawa analitumua kama tax. Tatizo likaanzia hapo.
Naomba niwaambie hivi mimi ni mama mwaminifu ninamwamini Mungu katika
kweli yote sikuwahi kumfikiria mume wangu vibaya au kama angaliweza kuwa
na mwanamke mwingine au kutembea na house girl nilikuwa namwamini sana
na nilikuwa bize sana nikidhani namsaidia mwenzangu kumbe wapi.
Gari lilianza kunionyesha mambo, mume akawa hataki kufanyia kazi akawa
anazunguka nalo tu, asubuhi naulizwa hela ya mafuta, matengenezo mpaka
nikajuta kununua hilo gari. Nikaamua kuwaambia ndugu zake waongee nae.
Walipoongea nae yeye akasema hawezi kuendesha taxi kama nataka ninunue
fuso ndio atafanya kazi hiyo, hilo likaniwia gumu nikachukua gari
nikampa dereva mwingine. Jamani! wakati mimi ninahangaika kutafuta pesa
za matumizi na kusomesha watoto kumbe mwenzangu kaanzisha uhusiano na
dada wa nyumbani ndio maana hata kazi hataki kufanya ila mimi nilikuwa
sijui kinachoendelea.
Mwaka 2003 tulianza kujenga na yeye ndio
alikuwa anasimamia ujenzi ila cha moto nilikiona, tunapanga bajeti ya
site vizuri namkabidhi pesa akirudi jioni ana shoti laki 2 au laki
inategemea na wingi wa pesa utakayompatia lazima apunguze materials bila
sababu mpaka nikaanza kumchunguza.
Hapo tulikuwa tunaishi
Kinondoni kumbe bila mimi kujua alikuwa kampangishia mwanamke chumba
huko Gongo la Mboto. Tukaanza kukorofishana maana ukiweka hela ndani
yeye kazichukua hata simu anabeba.
Alivyojua kuwa najua habari
za huyo mwanamke akaanza kusema mimi nataka kumwacha kwasababu hana
kazi, oh sababu unajenga na mambo mengi mabaya kwa kweli. Tulisuluhishwa
lakini hakuwa tayari kuacha tabia ya wanawake wa nje na mimi
nilimchukia sana kwa tabia zake ndicho kilichotutenganisha mimi na huyo
mume wangu.
Tulipoamua kutengana aliniambia niondoke na watoto
niliondoka nao na wanasoma vizuri tu kwani niliamua kuwapeleka Boarding
School ili wasiadhirike na kutengana kwetu japokuwa wakirudi likizo Mume
wangu anakuja kuwaona lakini hawasaidii kwa chochote hata chupi
hawanunulii.
Kwa sasa anafanya kazi nzuri tu lakini hataki
kuwasaidia watoto. Mwaka huu kabla watoto hawajarudi Shuleni waliniomba
sana nimsamehe baba yao na nilifikiri sana nikawaita wazee na
nikawaambia kuwa nimemsamehe kilichotushangaza ni kwamba yeye hajakubali
kusamehewa anachotaka ni nyumba niandikwe kwa jina lake kwanza na gari
ninalotumia nimpe au niliuze ndio atarudi.
Kwa masharti hayo
mie nimesema basi na kila mtu aishi peke yake maana naona mwenzangu
anawivu na nilichonacho ambacho kimsingi ni cha familia yetu, nimeogopa
masharti yake maana anaweza kutufanya tuanze kupanga tena.
Kinamama ninachotaka kujua ni hiki; Kwa kina mama hivi waume zenu nao
wakijua kuwa umejua anachokukosea na kutengana huwa wanawasusia familia?
..... na kina baba naomba kuwauliza mpaka lini mtawatesa wake zenu kwa kuwasusia familia zenu?
pole dear mama,,!!!
ReplyDelete